MKWASA ‘AIMWAGA’ YANGA, SASA STARS KIMOJA, STARS KAMILI
KUIVAA MALAWI JUMATANO!
Charles Boniface Mkwasa amepewa mkataba wa kudumu kukinoa
kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kwa kipindi cha mwaka mmoja
na nusu kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu na kumalizika Machi 31, 2017.
TFF Imefikia makubaliano hayo na
kocha Mkwasa baada ya kurudhika na utendaji wake katika kukinoa kikosi cha timu
ya Taifa, ambapo mpaka sasa ameweza kuingoza Stars katika sare ya michezo
miwili dhidi ya Uganda na Nigeria.
Kufuatia kusaini mkataba huo, Mkwasa
atapatiwa huduma na marupurupu yote aliyokuwa akipewa kocha aliyeondoka.
Naye kocha Mkwassa ameeleza
kufurahishwa na makubaliano haya na ameahidi kufanya kila jitihada kuhakikisha
kiwango cha Timu ya Taifa kinapanda.
Aidha Kocha Mkwassa ametoa wito kwa
wadau wa mpira kumpa ushirikiano katika majukumu yake mapya.
STARS YAKAMILIKA KUIVAA
MALAWI KESHO
Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)
inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, Charles Mkwasa amesema kikosi chake kipo
tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Malawi kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe
la Dunia mwaka 2018.
Mkwasa amesema kikosi chake kipo
kaika hali nzuri baada ya kufanya mazoezi ya mwisho leo asubuhi ambapo
wachezaji wote wapo katika hali nzuri wakiwemo wachezaji wawili Mbwana Samata
na Thomas Ulimwengu kutoka klabu ya TP Mazembe ya Congo DR.
“Tunatambua umuhimu wa mchezo wa
kesho, wachezaji wana ari na morali ya hali ya juu, kikubwa tunawaomba
watanzania wajitokeze kwa wingi uwanjani kuja kutu sapoti katika mchezo huo wa
kesho” Alisema Mkwasa.
Kwa upande wa kocha msaidizi wa
Malawi (The Flames), Ramadhan Nsanzurwimo amesema wanaiheshimu Tanzania,
wanatambua kesho kutakua na mchezo mzuri, na wao kama Malawi wamejiandaa vizuri
kwa mchezo huo.
IMETOLEWA NA:
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
Tanzania Football Federation – TFF
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KOMBE LA DUNIA 2018
Afrika-Raundi ya Awali
**Saa za Bongo
Jumatano Oktoba 7
15:30 Seychelles v Burundi
16:00 Tanzania v
Malawi
16:30 South Sudan v Mauritania
17:30 Mauritius v
Kenya
Alhamisi Oktoba
8
15:00 Comoros v Lesotho
18:00 Sao Tome And Principe v
Ethiopia
19:00 Liberia v
Guinea-Bissau
Ijumaa Oktoba 9
15:30 Somalia v
Niger
16:00 Djibouti v
Swaziland
20:00 Gambia v Namibia
Jumamosi Oktoba 10
14:30 Central African Republic v
Madagascar
16:00 Eritrea v Botswana
17:30 Chad v Sierra Leone
Marudiano
Jumapili Oktoba 11
15:00 Malawi v
Tanzania
16:00 Ethiopia v Sao Tome And
Principe
16:00 Kenya v
Mauritius
Jumanne Oktoba 13
14:30 Madagascar v Central African
Republic
16:00 Burundi v Seychelles
17:00 Sierra Leone v
Chad
18:00 Namibia v Gambia
18:00 Niger v
Somalia
19:00 Lesotho v Comoros
19:00 Guinea-Bissau v
Liberia
20:00 Botswana v Eritrea
20:00 Swaziland v
Djibouti
20:00 Mauritania v South Sudan
No comments:
Post a Comment