HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Wednesday, 7 October 2015

SERIKALI IJAYO YATAKIWA KUBORESHA MALEZI YA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA HATARISHI.



NA .REBECA DUWE .LUSHOTO
Ikiwa zimebaki siku chache  za  watanzania kufika katika vituo vya kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa ngazi ya  Urais , Wabunge na Madiwani, Serikali ya awamu ya tano inayotarajiwa kuingia madarakani baada ya uchuguzi mkuu oktoba 25 mwaka huu  imetakiwa   kuweka kipaumbele  katika  malezi ya watoto yatima na wale wanaoishi katika Mazingira hatarishi  wakiwemo walemavu wa aina zote ni ya kila mtu na sio lavituo maalum  na taasisi Fulani.

Hayo  yalisemwa na  mkuu wa kituo cha  kuwalelea watoto yatima  Irente kilichopo chini  ya Dayosisi ya kaskazini Mashariki Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT. bi.  Enna Mdemu wakati wa mahafali ya 47 ya chuo cha mafunzo  ya malezi bora na  makuzi ya watoto  Irente  kilichopo ndani ya kituo hicho.
Aidha alisema kuwa suala la malezi ya watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi ni jukumu la kila mtanzania  pamoja na  serikali kulivalia njuga na kulitazama kwa jicho pevu badala ya kuwaachia vituo maalumu na taasisi  Fulani .

Alisema kuwa serikali ndio ina jukumu kubwa la kuwaelimisha , kuwahamasisha wananchi kushiriki katika kutoa michango mbalimbali katika malezi ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ikiwa ni pamoja na kuwasaidi wale wasiojiweza.

“ Ni wakati wa kila kiongozi au mwamnachi wa kawaida kuwa na muda kuwaza kusaidia watoto yatima na waishio katika mazingira hatarishi ili wapate kuishi kama watoto wengine bila kuangalia kabila wa rangi kwani kwa kufanya hivyo taifa litabarikiwa.” Alisema Mdemu.

Kwa upande wake mgeni rasmi ambaye mkurugenzi wa huduma za jamii katika Dayosisi hiyo Mch. Joycy Kibanga aliwataka  wahitimu hao wa Chuo cha mafunzo ya malezi bora na makuzi ya watoto   kuwa mfano wa kuigwa katika Jamii kutokana kile walichokijifunza kuwalea watoto wachanga hadi kukua lakini pia kutunza watoto bila ubaguzi pamoja na mambo mengine mazuri waliyoyajifunza.
Aidha aliwataka kutokurudi nyuma na kujisahau kuwa wao ni kioo cha jamii popote waendapo ni msaada mkubwa  toafuti na wale ambao hawajapitia chuo hicho.Chuo hicho cha mafunzo ya malezi bora na makuzi  ya watoto  kimefanikiwa kuwaaga  Wahitimu wapatao 12 kumi na  mbili  ambao ni wasichana waliokuwa wakijifunza mambo mablimbali  yahusuyo  standi za maisha hususani jinsi ya  malezi bora na makuzi ya watoto.

Aidha Dayosisi hiyo licha ya kuwa na kituo hicho cha watoto yatima pia kuna vituo vingine viwili vinatunzwa na DKMS  hapo Irente ikiwemo kituo cha watu wasioona , wenye uoni hafifu Irente na  kituo cha watoto wenye ulemavu wa akili Irente
Mwandishi Wetu amepata fursa ya kutembelea vituo vyote vitatu  na kuona changamoto mbalimbali zilizopo vituoni hapo ,kikubwa ikiwa  ni ufinyu wa bajeti, kutokupata ruzuku serikalini na misaada maalumu inayotolewa kitaifa  kusaidia watoto kwa yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ,uchakavu mabati ya mabweni ya wanachuo  katika kituo cha watoto  yatima Irente.

Hata hivyo bi, Mdemu alisema kuwa ktuo hicho kinawapokea watoto baada ya mfiwa kupata utambulisho wa serikali  ya kijiji  kusajiliwa na ustawi wa jamii na kupimwa na mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya ,iwapo afya yake  ni nzuri au au anahitaji matibabu kwanza .
Alisema kuwa sera ya Taifa na kanisa ni kuwalea watoto hapo kituoni kwa  miaka miwili  kisha ndugu au walezi wanawachukua na kukaa nao  nyumbani .

Kwa uapnde wa kituo cha kuwalelea wenye ulemavu wa akili, mkuu wa kituo hicho mwl.Yasin Shehagilo alisema changamoto kubwa ni Dhana potofu kwa wanajamii  kuamini kuwa watu wenye uleamavu wa akili hawawezi kufanya kitu chochote  jambo ambalo limechangia kutengwa  kwa wenye uleamavu wa akili.
Aidha pia ameiomba jamii  ione umuhimu wa kuwalea watoto wenye uleamvu wa akili na kuwachukulia kama wengine bila kwadharau kwani wakifundishwa wanaelewa na wanaweza kufanya kazi nzuri tofauti wanavyofikiriwa.

Sambamba na hayo ameiomba serikali iweze kutengeneza miundo mbimu ya shule kwa watoto  wenye ulemavu na kuboresha shule zilizopo ziwe  na vyoo  rafiki  kwa mazingira ya walemavu bila kupata madahara yeyote.

Vilevile na kituo cha wasioona  kina kilio cha  kuboreshwa kwa miundo mbinu  kama wanafunzi hao pamoja na vifaa vya kufundishia wanafunzi hao , suala ambalo limeelekezwa kwa serikali kuliangalia kwa jicho pevu ili kuweza kuwasaidia walemavu waliopo  katika jamii wapete elimu bora na satahiki.

No comments:

Post a Comment