IMEFAHAMIKA kuwa
jamii ya wanawake nchini inaendelea kuwa kandamizi kutokana na uelewa mdogo wa
masuala ya kisheria hali inayopelekea wengi kukosa haki zao.
Hayo
yamefahamishwa na mwanasheria kutoka asasi isiyo ya kiserikali TEWOREC, Victor Kisaka wakati
akizungumza kupitia kipindi cha TUZUNGUMZE asubuhi kinachorushwa na redio
huruma kila jumatatu hadi ijumaa.
Kisaka
amesema kuwa hali hiyo ya uelewa mdogo inachangiwa zaidi na idadi ndogo ya wanasheria nchini lakini pia wananchi wengi
hawana utaratibu wa kusoma ili kujielimisha kuhusu sheria inavyoelekeza dhidi
ya haki zao.
Akifafanua
zaidi na kujikita katika sheria ya ndoa ya
mwaka 1971 sura namba 29, ametolea mfano kwa jamii ukanda wa pwani
wanawake wamekuwa wakilea familia na hata kudiriki kuwahudumia waume zao wenye
nguvu na uwezo wa kufanya kazi na wengine kufungiwa kabisa wasijishughulishe
bila kujali kuwa ni kadhia kwao.
Kadhalika
mwanasheria huyo amebainisha kuwa sheria hiyo aimkatazi mwanamke kuhudumia
familia pale inapoonekana mwanaume hana uwezo wa kuzalisha, hivyo ametoa rai
kwa pande zote kujishughulisha na kusaidia jukumu la malezi kwa ustawi wa
familia zao na jamii kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment