Jamii imeaswa
kuwafichua madereva wa pikipiki wanaovunja sheria za usalama barabarani,
wanaoendesha kwa fujo na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa njia ndogo za
mitaa na kusababisha ajali na hata vifo huku waathirika wakubwa wakiwa ni
watoto, walemavu, wagonjwa na Wazee.
Hayo
yamesemwa na Mkufunzi wa chuo cha Mafunzo ya Udereva na Ufundi Stadi(C.U.H) cha
jijini Tanga Mwl Mggalu wakati akizungumza na kituo hiki Ofisini kwake kuhusu
umuhimu wa mafunzo kwa madereva wa vyombo vya usafirishaji kwa njia ya barabara
yaani pikipiki na Magari.
Mwl
Mggalu amesema ni wakati sasa jamii kutambua athari za utumiaji holela wa
vyombo hivyo kwani watu wengi wamekuwa wakipoteza mali, kupata ulemavu wa
kudumu na hata vifo kutokana na ajali zinazosababishwa na madereva wapikipiki
ambao ni wazembe na wasiojua sheria za usalama barabarani.
Aidha
ameliomba jeshi la Polisi kikosi cha Usalama barabarani nchini kubadili adhabu
ya faini na kuwa kifungo kwa madereva wanakamatwa kwa uvunjaji wa sheria za
usalama barabarani ili iwe fundisho kwa wengine wanaomudu kulipa faini na
hatimaye wanaendelea kuwa chanzo cha ajali nchini.
No comments:
Post a Comment