AZAM KAMA YANGA “YAENDELEZA DOZI KWA MBEYA CITY”
Kikosi cha Azam FC kimeendeleza ushindi katika Ligi Kuu Bara baada ya kushinda
kwa maba 2-1 dhidi ya Mbeya City katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Azam
Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.
Azam
ilianza Ligi Kuu Bara kwa kuichaa Prisons bao 2-1, ikaendeleza kipigo cha 2-0
kwa Stand United kabla ya kuitandika Mwadui FC 1-0.Sasa ina pointi 12 sawa na
Yanga na Mtibwa Sugar ambazo hazijapoteza hata mechi moja katika nne
zilizocheza.
Mabao
ya Azam FC katika mchezo huo yalifungwa na kiungo Mudathir Yahya katika dakika
ya 11 kabla ya Kipre Tchetche kumaliza kazi katika dakika ya 52.Hata hivyo,
Mbeya City walijitutumua na kupata bao katika dakika ya 55 kupitia kiungo wao
Raphael Alpha.
Hata
hivyo, dakika za mwisho Mbeya City walionekana kukaa vizuri zaidi na
kuwahenyesha Azam FC ambao hata hivyo safu yao ya ulinzi ikiongozwa na Serge
Wawa ilionekana kusimama imara.
WANA KIMANUMANU WAPATA USHINDI WA KWANZA TANGA
African Sports imeamka
baada ya kupata ushindi wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu Bara.African Sports
imeibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi ya ligi hiyo dhidi ya Ndanda FC.Katika
mechi hiyo kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, wageni walionekana kuwa
imara zaidi kipindi cha kwanza.
Hata hivyo, wenyeji African Sports
walijibu mapigo baada ya kuanza kipindi cha pili kwa kasi hadi walivyopata bao.Bao
lao lilifungwa na Hassan Matelema katika dakika ya 59 kupitia Hassan Matelema.
Baada ya bao hilo, Ndanda walicharuka
lakini mara kadhaa African Sports ambao walicheza kwa tahadhari kubwa walikuwa
wakijibu mapigo.Kabla Sports ilicheza mechi tatu na
kupoteza zote, ikianza kufungwa bao 2-0 na Simba, ikasafiri hadi Shinyanga na
kufungwa tena kwa idadi hiyo na Mwadui.
Kabla ya mechi ya leo, ilibaki
Shinyanga safari hii kwenye Uwanja wa Kambarage, ikachabwa na Stand United bao
2-o.
TFF YATUMA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA YA MCHEZAJI WA COASTAL ALIYEFIA
UWANJANI MKWAKWANI.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
limetuma salam za rambirambi kwa mwenyekiti wa klabu ya Coastal Union, Dr Twaha
Ahmed kufuatia kifo cha mchezaji Mshauri Salim aliyefariki jana jioni jijini
Tanga.
Katika salam hizo za Rais wa TFF Jamal Malinzi kwenda
kwa uongozi wa klabu ya Coastal Union, amewapa pole wafiwa ndugu jamaa na
marafiki pamoja na uongozi wa klabu hiyo na kusema TFF wako nao pamoja katika
kipindi hichi cha maombelezo.
Marehemu Mshauri Salim alikuwa mchezaji wa kikosi cha
vijana (U20) cha Coastal Union, alifariki jana jioni wakati akipelekwa
hospitali baada ya kuanguka uwanjani wakati wa mchezo wa utangulizi wa timu
yake dhidi ya timu ya Eagle Academy ya jiji humo.
Kabla ya umauti kumfika, Mshauri aligongana na
mchezaji wa timu ya Eagle Academy na kutolewa nje kwa matibabu, ambapo aliweza
kurudi uwanjani na kuendelea na mchezo huo kabla ya kuanguka peke yake tena
uwanjani na kufariki akiwa njiani kupelekwa hospitalini.
KIATU CHAKAVU CHA MSHAMBULIAJI WA SIMBA GUMZO MITANDAONI
Kiatu cha mshambuliaji
mpya wa Simba, Pape Ndaw raia Senegal kimekuwa gumzo kupita kiasi mitandaoni.Mshambuliaji
huyo aliingia katika mechi hiyo kuchukua nafasi ya Hassan Kessy wakati Simba
ikiivaa Yanga na kupoteza kwa mabao 2-0.
Ndaw ambaye urefu wake ni futi 6.6 na
ndiye mchezaji mrefu zaidi katika Ligi Kuu Bara, alionekana akiwa amevaa kiatu
aina ya Adidas chenye rangi nyeupe na bluu kikiwa kimechakaa kwelikweli.
Kiatu hicho ‘kilivutwa’ na runinga ya
Azam TV na kuzua gumzo kwelikweli.
Uchakavu wa kiatu hicho ambacho
ukubwa wake utakuwa zaidi ya namba 12, kilionekana kuchoka utafikiri wachezaji
wa ‘mchangani’.
Kuanzia hapo, mashabiki wa Yanga
wameanza kuwadhihaki wenzao wa Simba kwamba wamesajili mchezaji ambaye hana
hata fedha ya kununua kiatu tu!Wengi walikuwa wakiwatania Simba na kuwaambia
‘wamepigwa’ hawezi kuwa ana mawasiliano au mkataba na Steau Bucharest ya
Romania wakati hata kiasi tu hawezi kununua tena katika mechi kubwa kama hiyo.
Baadhi ya mashabiki wa Simba walikuwa
wakijibu mapigo kwamba kununua kiatu si kazi ya klabu, badala yake mchezaji
mwenyewe.
MANARA ALIA NA MWAMUZI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tarehe 26-9-2015 jana
Jumamosi kulifanyika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara baina ya timu yetu ya
Simba Simba dhidi ya timu ya Yanga.
Kwenye mchezo huo timu yetu imepoteza
mchezo huo kwa kufungwa bao 2-0.Tumeanza kuandika hivyo hapo juu kwa makusudi
kuonyesha sisi Simba tumeyakubali matokeo hayo ya dakika 90 za mchezo na
tutumie nafasi hii kiungwana kabisa kuwapongeza watani wetu wa jadi kwa ushindi
huo walioupata.Pili tumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kumaliza mchezo huo
salama, na hapa Mungu ashukuriwe sana pamoja na wapenzi wetu pia.
Sababu washabiki wetu wameonyesha
utulivu wa kiunamichezo kwa kutokufanya fujo yoyote licha ya mwamuzi wa mchezo
huo Israel Nkongo kuharibu mchezo kwa makusudi.Nkongo kwa dhamira ya kusudi jana aliamua kuwatoa wachezaji wetu
mchezoni kwa kuanza kugawa kadi kwa wachezaji wetu pasi na sababu na kwa rafu
zilezile kuacha wachezaji wa Yanga kucheza bila kuwaonya.
Kilichoshangaza washabiki wote
waliokuwa uwanjani na walioangalia kwenye televisheni ni kumuacha mchezaji wa
Yanga Donald Ngoma kuendelea na mchezo ilhali alimpiga kichwa cha maksudi
mchezaji wetu Hassan kessy!Mbali ya vitendo hvyo wachezaji wetu wametulalamikia
kutukanwa na mwamuzi wa mchezo huo Nkongo.
Tunaamini TFF watachunguza malalamiko
yetu na kuchukua hatua stahiki kwa mwamuzi huyo ambaye kila mtu aliyeuona
mchezo huo anakiri kuwa alishindwa kuumudu.Mwisho na kwa umuhimu wa kipekee
klabu ya Simba inaendelea kuwashukuru washabiki kwa utulivu wao licha ya
vitendo vya mwamuzi huyo ambavyo vingeweza kabisa kuharibu amani iliyokuwepo
uwanjani jana.
Tunawaomba waendelee kuwa watulivu
katika kipindi hiki ambacho uongozi wenu umewaandikia TFF na bodi ya ligi
ambazo tunaamini zitatenda haki.
Reclaming our glrory
Simba Nguvu Moja
Imetolewa na Haji
S.Manara
Mkuu wa Habari wa Simba
Simba Sports Club
KIPIGO KWA RUVU KOCHA MINZIRO ABWAGA MANYANGA
Kocha wa JKT Ruvu, Fred Felix
Minziro, amebwaga manyanga.Minziro anaondoka, mechi yake ya mwisho ikiwa ni
dhidi ya Stand United waliolala kwa bao 1-0 lililofungwa na straika nyota wa
zamani wa Simba, Elius Maguri.
Minziro ameachia ngazi katika nafasi yake hiyo baada ya kuona mwenendo
wa kikosi chake si mzuri katika Ligi Kuu Bara.Kocha huyo ameamua kuachia ngazi
saa chache baada ya JKT kupokea kipigo cha bao 1-0 dhid ya Stand United tena
JKT wakiwa nyumbani, jana.Katibu Mkuu wa JKT, Ramadhani Madoweka amesema kweli
Minziro ameachia ngazi.
“Kweli Minziro ameachia ngazi, timu
sasa iko chini ya Greyson Haule,” alisema.
JKT iko njiani kwenda mkoani Tabora ambako ina kibarua kingine kigumu
dhidi ya Kagera Sugar ambayo inatumia Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.Hadi Minziro
anaondoka alikuwa ameongoza timu hiyo katika mechi nne, akianza ugenini dhidi
ya Majimaji mjini Songea ambako walilala kwa bao 1-0.
Baada ya hapo, wakasafiri kwenda Mbeya ambako walichapwa bao 3-0 na
Prisons kabla ya kutua jijini Dar es Salaam walipokutana na kipigo cha paka
mwizi cha mabao 4-1 dhidi ya Yanga na jana, wakiwa nyumbani kwa mara ya kwanza,
wakadundwa 1-0 na Stand.
No comments:
Post a Comment