Mshambulizi hodari zaidi
duniani Lionel Messi wa Barcelona hatashiriki mashindano yeyote kwa majuma 8
yajayo kufuatia jeraha la goti.Mshambulizi huyo wa Argentina aliumia katika
mechi ya ligi kuu ya Uhispania dhidi ya Las Palmas.Barcelona ilishinda mechi
hiyo mabao 2-1.
Messi
mwenye umri wa miaka 28 aliondolewa uwanjani na kukimbizwa hospitalini kunako
dakika ya 3 ya mechi hiyo.Hata hivyo huenda mshindi huyo wa tuzo la mchezaji
bora duniani akarejea katika mechi ngumu baina ya Barcelona na wapinzani wao wa
jadi Real Madrid tarehe 22 Novemba.
Kocha
Luis Enrique alisema kuwa atajitahidi kuendeleza mfumo wa mchezo wao hata bila
ya messi kuwepo.
''Kutokuwepo
kwa messi ni pigo ila tutalazimika kujifunga kibwebwe, na hili ninamaanisha
kila mchezaji wetu atajikaza kisabuni ilikuziba pengo hilo japo ni kubwa...''
Image
copyright AP Image caption Ronaldo amecheza mechi 3 bila ya kufunga bao lolote
''Unajua
vyema kuwa messi si mchezaji wa kawaida, mara nyingi amekwamua safu za ulinzi
za timu nyingi wakati ambao hata mimi mwenyewe nahisi nimejitolea mzima
mzima.'' Alisema Kocha Luis Enrique.
Licha
ya kuondoka kwake mapema uwanjani, mshambulizi mwenza wa Barca,Luis Suarez
alijifurukuta na kuwafungia mabingwa hao mabao mawili muhimu na kuisaidia
kurejea kileleni mwa jedwali la la liga.Real Madrid walijipata taabani pia
baada ya kushindwa kufaidi uwanja wa nyumbani ,walipotoka sare tasa na Malagaat
katika uga wa Bernabeu.
Villarreal
kwa upande wao waliwazima mabingwa wa mwaka wa 2014 Atletico Madrid bao moja
kwa nunge.
No comments:
Post a Comment