Mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la Abdu Ngodasa mwenye umri wa miaka 27 mkazi
wa Mlingano Wilayani Muheza amefariki dunia baada kupigwa na fimbo kichwani .
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Tanga Zuberi mwombeji
alisema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 27 September mwaka huu majira ya saa
tano usiku katika maeneo Mlingano Wilayani Muheza mkoani hapa.
Alisema
Marehemu aliuawa na mtu aliyefahamikia kwa jina la Andrew Mwakapola umri wa
miaka 54 baada ya kunywa pombe nyingi na kulewa ndipo wakaanza kupigana na
kusababisha kifo cha mwenzake.
Hata hivyo
Kamanda Mwombeji alitoa wito kwa wananchi wote wa mkoa huo kuacha kunywa pombe
kupita kiasi hali ambayo inayopunguza nguvu kazi ya Taifa.
Aidha
aliwapongeza wananchi wa mkoa wa Tanga
kwa kudumisha amanina kuwataka kuendelea
kuwa watulivu hasa kwa kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu ujao mpaka
uchaguzi utakapomalizika.
No comments:
Post a Comment