STAA wa Bayern Munich Robert Lewandowski Jana alipiga Bao 5 ndani ya Dakika 9 na kuvunja Rekodi kadhaa za Bundesliga baada ya Timu yake kuitwanga VfL Wolfsburg Bao 5-1.
Katika Mechi hiyo iliyochezwa huko Allianz Arena huko munich, Germany, Wolfsburg waliongoza 1-0 hadi Mapumziko.
Kipindi cha Pili Robert Lewandowski, Mchezaji kutoka Poland mwenye Miaka 27, alitumia Dakika 4 tu kupiga Hetitriki ikiwa ndio Hetitriki iliyofungwa ndani ya muda mfupi katika Historia ya Bendesliga.
Rekodi hii ilikuwa ikishikiliwa na Mchezaji wa Duisburg, Michael Toennies, aliyoweka Mwaka 1991 kwa kufunga Hetitriki ndani ya 5.Pia Lewandowski, kwa kupiga Bao 5 ndani ya Dakika 9 za Kipindi cha Pili, ameivunja Rekodi ya Jermaine Defoe wa Tottenham ya kufunga Bao 5 ndani ya Dakika 36 ya Kipindi cha Pili wakati Tottenham inaitwanga Wigan 9-1 Mwaka 2009.
Bosi wa Bayern Pep Guardiola alipigwa butwaa na Rekodi ya Lewandowski na kubaki kusema: 'Mara nyingine Soka ni Wehu!'
BUNDESLIGA
RATIBA/MATOKEO
Jumanne
Septemba 22
Bayern Munich 5 VfL Wolfsburg 1
Hertha Berlin 2 Cologne 0
Ingolstadt 0 Hamburg 1
Darmstadt 2 Werder Bremen 1
Jumatano
Septemba 23
**Saa
za Bongo
Schalke 04 v Eintracht Frankfurt
Bayer Leverkusen v Mainz
Borussia Moenchengladbach v Augsburg
Hanover 96 v VfB Stuttgart
Hoffenheim v Borussia Dortmund
No comments:
Post a Comment