AARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Moto
mkubwa umezuka mwishoni mwa wiki hii na kuunguza sehemu ya Mlima Meru katika
Hifadhi ya Taifa ya Arusha. Taarifa za awali zinaonyesha kuwa chanzo cha moto
huo ni vitendo haramu vya urinaji wa asali ndani ya msitu wa hifadhi hiyo.
Wananchi wapatao 200 kutoka
vijiji jirani vya Olosinoni na Kisimiri Juu wakishirikiana na TANAPA
wamefanikiwa kuudhibiti moto huo ili usiweze kuleta madhara makubwa kwa
binadamu hususan wageni wanaotembelea hifadhi kwa lengo la kupanda Mlima Meru.
Hadi sasa hakuna wageni
waliodhurika na moto huo na tahadhari zote zimechukuliwa ili kudhibiti madhara
zaidi kwa binadamu na shughuli za utalii ndani ya hifadhi.
Shirika la Hifadhi za Taifa
linaendelea kuwatahadharisha wananchi juu ya vitendo vya kuingia ndani ya
hifadhi bila kibali kwa shughuli ambazo zinaweza kuwa chanzo cha kuzuka kwa
mioto hii ambayo husababisha uharibifu wa mazingira pamoja na kuharibu vyanzo
vya maji.
Aidha, katika kuhakikisha kuwa
moto huo unadhibitiwa kwa haraka, TANAPA imeongeza nguvu kazi ya wananchi
wakishirikiana na vyombo vingine vya dola ili kuweza kuudhibiti moto huo.
Mwisho, taarifa kamili juu
madhara yaliyosababishwa na moto huo itatolewa mara baada ya kukamilika kwa
zoezi la kuzima moto na umma utaendelea kupewa taarifa ya maendeleo ya zoezi la
uzimaji wa moto kila wakati.
Imetolewa
na Idara ya Mawasiliano
HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA
21.09.2015
dg@tanzaniaparks.com
www.tanzaniaparks.com
HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA
21.09.2015
dg@tanzaniaparks.com
www.tanzaniaparks.com
No comments:
Post a Comment