HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Thursday, 17 September 2015

NIMEKUWEKEA HAPA TAARIFA ZOTE ZA LIGI KUU YA SOKA TANZANIA BARA. MATOKEO , MSIMAMO NA RATIBA.


Mgambo jkt
0
 : 
2
Simba sc

Mwaka huu kazi ipo, wekundi wa msimbazi simba sc kwa mara ya kwanza amefanikiwa kuvuna pointi 6 katika uwanja wa mkwakwani baada ya jana kufanikiwa kupata ushindi wa pili mfululizo katika uwanja wa mkwakwani mkoani tanga.

Simba sc jana wameifunga jkt mgambo goli 2-0 katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu tanzania bara ambapo leo michezo yote 8 ilichezwa katika viwanja 8 tofauti.
Simba sc walianza kusheherekea ushindi wao katika dakika ya 28 kupitia kwa justice majabvi, goli ambalo liliwapeleka simba sc mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0.

Mtoke benchi hamisi kiiza akichukuwa nafasi ya mwingi kazimoto aliiandikia simba sc goli la 2 katika dakika ya 73 na kuihakikshia simba sc ushindi wa kwanza mbele ya mgambo shooting katika uwanja wa mkwakwani.

Hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa simba sc walikuwa mbele kwa goli 2-0 na kupelekea kufikisha pointi 6 katika msimamo wa ligi kuu ya vodacom.

Mbeya city
3
 : 
0
Jkt ruvu
Jkt ruvu wameendeleza jinamizi la kupoteza mchezo baada ya jana kukubali kichapo cha pili mfululizo toka kwa mbeya city, ambayo nayo ilipoteza mchezo wake wa kwanza.
Katika mchezo wa leo mbeya city walianza kuandika goli lao la kwanza katika dakika ya 25 kupitia kwa joseph mahundi goli liliowapeleka mbeya city mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0.

Katika kipindi cha pili mbeya city walifanikiwa kufunga magoli mawili yaliyofungwa na themi felix katika dakika ya 56 kwa mkwaju wa penati, na jingine kupitia david kabole katika dakika ya 68.mpaka dakika 90 zinakamilika mbeya city walikuwa mbele kwa goli 3-0 na kufanikiwa kujikusanyia pointi zake tatu katika uwanja wake wa sokoine ya mbeya.

Yanga
3
 : 
0
T.prisons
Mabingwa wa ligi kuu ya vodacom yanga wameendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya vodacom baada ya kufanikiwa kuichapa tanzania prisons goli 3-0, katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa taifa jijini dar es salaam.

Katika mchezo wa jana yanga sc walianza kupata goli kupitia kwa mbuyu twite aliyemalizia mpira alio utema kipa wa prisons mohamed yusuf katika dakika ya 30.
Wakati timu zinajiandaa kwenda mapumziko amisi tambwe aliiandikia yanga goli la pili katika dakika za nyongeza na kuipeleka yanga mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-0.

Kipindi cha pili kilirejea kwa kasi, huku prisons wakisaka goli, wakati yanga wakisakata soka safi na kusaka goli lazidi ndipo katika dakika ya 59 yanga walipata penati iliyopigwa kwa ufasaha na donald ngoma na kuipa yanga ushindi wa goli 3-0.

Yanga sc wamefikisha pointi 6 wakiwa na magoli 5 ya kufunga huku wakiwa bado hawajaruhusu goli katika nyavu zake na kujikuta wakiwa kileleni mwa ligi.

Matokeo ya mechi za jana kwa ujumla. 2015-09-16
Ft
Yanga
3
 : 
0
T.prisons
Ft
Mgambo jkt
0
 : 
2
Simba sc
Ft
Majimaji
0
 : 
0
Kagera sugar
Ft
Mbeya city
3
 : 
0
Jkt ruvu
Ft
Stand united
0
 : 
2
Azam fc
Ft
Toto africans
1
 : 
2
Mtibwa sugar
Ft
Ndanda fc
1
 : 
0
Coastal union
Ft
Mwadui fc
1
 : 
0
African sport
Michezo inayokuja
2015-09-19
16:00
Stand united
Vs    
African sport
16:00
Mgambo jkt
Vs    
Majimaji
16:00
T.prisons
Vs    
Mbeya city
16:00
Yanga
Vs    
Jkt ruvu

2015-09-20
16:00
Mwadui fc
Vs    
Azam fc
16:00
Mtibwa sugar
Vs    
Ndanda fc
16:00
Simba sc
Vs    
Kagera sugar
16:00
Coastal union
Vs    
Toto africans















No comments:

Post a Comment