NA REBECA DUWE, TANGA.
KITUO cha vijana Mafunzo na
maadili Novelty Jijini Tanga (NOVELTY YOUTH CENTRE TANGA)
kinachomilikiwa na Kanisa la Free Pentekoste Church of
Tanzania (FPCT ) Jijini Tanga kimefanya Tamasha la mashindano ya uandishi
wa Insha kwa wanafunzi wa shule za msingi jiji la Tanga kwa mara ya
kwanza , na kupata washindi kumi waliobahatika kupata fursa za kusoma
bure program tofauti tofauti za kompyuta zinazofundisha katika
kituo hicho cha vijana Novelty.
Mkuu wa kituo
cha Vijana Novelty jijini Tanga
akiimba wimbo
wa kuwahamasisha vijana
katika maadili
kwenye Tamasha la uandishi wa Insha
lililoandaliwa
na kituo hicho.
|
Tamasha hilo limefanyika siku ya
jumatatu iliyopita kituoni hapo na kuwakusanya mamia ya wanafunzi kutoka
shule mablimbali za msingi kutika jiji la Tanga likiwa na lengo la kuwajengea
wanafunzi uwezo wa kujenga hoja za kiuandishi kuibua vipaji mablimbali
vya watoto na vijana ili kufikisha ujumbe kwa wahusika ili kutekeleza wajibu
wao.
Akizungumza wakati wa Tamasha hilo
Mkuu wa kituo hicho cha Novelty na mratibu wa Tamasha hilo Jasson
Ellyakimu alisema kuwa kusudi la kuandaa mashindano ya uandishi wa Insha
kwa wanafunzi wa shule za msingi ni kuangalia uwezo wao wa kufikiri
katika kufikisha ujumbe kwa hadhira kuhusu jambo Fulani na uelewa wao pia ili
kugundua maendeleo yao katika kujifunza masomo wakiwa mahuleni .
Alisema Insha hiyo ilikuwa
inahusu Viwanda, Rasilimali na vivutio vilivyoko ndani ya mkoa wa Tanga
vinawasaidia vipi serikali pamoja wakazi wa mkoa wa Tanga ili kupata
maendeleo, ambapo waliweka vigezo vya kuzingatiwa katika uandishi huo kwa
kuangalia Uelewa wa mwanafunzi mwenyewe na utafititi wake juu Rasilimali
hizo lakini pia jinsi ya kuifafanua mada mbele ya hadhara na yeye
mwenyewe kujieleza pamoja na muonekano wake binafsi.
Mkuu wa kituo cha Novelty na mratibu wa Tamasha uandishi wa Insha katika Shule za Msingi jiji la Tanga Jasson Ellyakim akimkabidhi zawadi mshindi wa pili Nasma Husein . |
Katika tamasha hilo la mashindano
hayo zilishiriki shule za msingi kutoka Kwa Kaheza ,Kana ,Kisosora, Mikanjuni,Donge,Kange
Kasera na Chuma ambapo mwanafunzi Mshindi wa kwanza alitokea shule ya msingi
Kange Kasera aliyeitwa Joshua Nikolaus Shemdoe umri wa miaka 13 na kupewa
zawadi ya sh.50,000 kesh na kupua nafasi ya kusoma bure progaramu
tatu za Kompyuta katika kituo cha Novelty ndani ya mwezi mmoja ,na
mwanafunzi wa pili alitokea Shule ya Msingi Mikanjuni aliyeitwa Nasma Husein
umri wa miaka 13 na kupewa zawadi ya 30,000 kesh na kupata nafasi
kusoma bure Program mbili za Kompyuta ndani ya wiki tatu kituoni hapo.
Na wanafunzi wote waliobaki ambao ni
mshindi wa tatu mpaka wa kumi walioshiriki uandishi wa Insha nao watosoma
bure Program moja moja ya kompyuta kwa ajili ya kuongeza
ujuzi wa Kutumia Kompyuta kituoni hapo.
Aidha Ellyakimu alisema tamasha hilo
litakuwa endelevu katika mkoa wa Tanga ili kusaka vipaji vya vijana walioko
mashuleni lakini pia kuwa hamasisha vijana kusoma kwa bidii na kwa ushindani
zaidi ili kuwapata waosomi weye uweledi wa mambo mengi
waliojengewa mwazo ya utafiti mapema katika Taifa.
Washiriki na washindi wa uandishi wa Insha kutoka shule tofautitofati wakiwa wamesimama mbele ya wanafunzi wenzao. |
Kwa upande wake Jaji mkuu wa
Mashindano hayo Jackson Amos ambaye ni mwalimu katika kituo hicho cha vijana
Novelty aliwapngeza washiriki wote na kuwataka kuongeza bidii katika uandishi
wa Insha pamoja masomo mengne mashuleni kwani hatua walioanza nayo ni nzuri kwa
sasa na inaonesha kuwa kuna wanafunzi wanaoweza utafiti wa hali ya juu endapo
watahamasishwa ipasavyo.
No comments:
Post a Comment