Wito umetolewa kwa
wakristo wakatoliki kumuomba Mungu ili waweze kuona kusikia na kutenda
katika maisha ya kumfuata kristu kwa Imani ya Kweli.
Hayo yamesemwa na Paroko wa Parokia ya Mt
PETRO Saruji Pongwe Pr Peter Bahati kwenye adhimisho la Ibada ya Misa Takatifu
ya Dominica ya 23 ya mwaka B kwenye kigango cha Mt Gerald Pongwe pia Ibada hiyo
ilikuwa ni maalum kwa Wanaume Wakatoliki kusherehekea sikukuu ya Somo wao Mt
Augustino.
Sambamba na hayo, Sherehe hiyo ilipambwa na
Wanaume wenyewe wakiwa wamevaa sare zao zenye maandishi yanayowatambulisha,
ambapo kwa pamoja walihusika kama waangalizi, walisoma masomo, maombi na kutoa
vipaji.
No comments:
Post a Comment