Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Tanga
Zuberi Mwombeji.
|
Akithibitisha
kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Zuberi Mwombeji amesema
ajali hiyo imetokea Sept 15 mwaka huu majira ya saa 5a asubuhi na kuhusisha
basi la Kamapuni ya Metro lanye namba za usajili T442 DFA aina ya SCANIA
lililokuwa likitokea Dar Es Salaam kuelekea Rombo Moshi mkoani Kilimanjaro
ambapo gari hilo lilipofika kwenye kona na lilihama njia na kutumbukia kwenye
mtaro.
Kamanda
Mwombeji amewataja waliofariki kuwa ni wanaume watatu waliotambuliwa kwa majina
ya Elimringi Minja 50 mchaga mkazi wa Moshi, Innocent Shayo 49 na Zakaria
Kitumpa 43mkazi wa Korogwe.
Wengine
ni Dezio Minja 47 mkazi wa Moshi na Mtoto Haika Elimringi 12 ambaye pia ni
mkazi wa Moshi mkoani Kilimanjaro.
Majeruhi
wa Ajali hiyo walipelekwa katika Hospitali ya Mkata kupatiwa matibabu huku 30
kati yao wakiruhusiwa na wengie 9 bado wanapatiwa matibabu.
Aidha
Kamanda amesema Dereva wa basi hilo aliyefahamika kwa jina la Raymond Frank
Urio ametoroka na jitihada za kumtafuta zinaendelea.
Jeshi
la Polisi mkoani Tanga linashukuru ushirikiano waliotoa wananchi wa maeneo ya
jirani kwa kusidiana na askari wa usalama kulinda mali za abiria wa basi hilo
kwani hakuna kilicho potea katika ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment