Imeelezwa kuwa Upendo na utii ndiyo nguzo ya
maisha ya mkristu katika kuimarisha ndoa kutenda haki ndani ya familia jamii na
taifa kwa ujumla.
Hayo yamesemwa na Katibu msaidizi ambae pia
ni mwanasheria wa jimbo na jimbo katoliki la Tanga Padre Ernest Kipingu kwenye
adhimisho la ibada ya misa takaifu ya dominika ya 21 mwaka B kwenye kanisa kuu
la mtakatifu Anthony wa padua chumbageni tanga.
Amesema katika maisha ya kila siku hasa ya
ndoa upendo unatakiwa kutawara nakuimalisha familia kwa muda wote kama mwanzo wa uchumba
ili kuweza kuwalea watoto katika imani ya kweli.
Hata hivyo padre kipingu amewahasa wakristu wote nchini kutokubali watu wanaojiinua na kutawana utashi wa mwingine
kwa nguvu zaidi pengine kutumia nguvu za jiza kuweza kukutumia na kukuongoza
kwa mapenzi yake bali nikumtegemea mungu kwa kusali na kuomba mapenzi ya mungu
yatimie kwenye maisha yetu ya kumfuasa kristu aliye hai.
No comments:
Post a Comment