Na Masanja Mabula.ZANZIBAR Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema kuwa ujenzi wa minara ya majaribio ya umeme wa
kutumia upepo na jua ni hatua za kukabiliana na tatizo la kukatika katika kwa
nishati ya umeme visiwani humo .
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Idd amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa minara hiyo kutaondoa tatizo
la kukatika katika umeme .
Kauli hiyo ameitoa wakati alipotembelea
ujenzi wa mnara wa umeme wa kutumia upepo na jua katika shehia ya Kiuyu Mbuyuni
Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba unaojengwa kwa ushirikiano kati ya
SMZ na Jumuiya ya Nchi ya Ulaya (EU).
Amesema kuwa mradi huo pia utapunguza gharama
za kulipia huduma hiyo na kuongeza kwamba wananchi wengi watamudu kutumia
huduma hiyo na hivyo kukuza uchumi na kuongeza kipato cha familia zao .
Aidha Seif ametumia fursa hiyo kuiwataka
wananchi wa shehia hiyo kushirikiana na watendaji wa Shirika la Umeme Zanzibar
(ZECO) ili kufanikisha ujenzi wa mnara huo .
Makamo wa pili wa Rais amewataka wananchi
kuwa wastahamilivu na kuacha utafiti ufanyike ili kubaini ni aina gani ya umeme
unafaa na ambao hautaathiri mazingira .
Akitoa maelezo ya ujenzi wa mnara huo kwa
Makamo Meneja Mradi Maulid Shirazi Hassan amesema kuwa Jumla ya minara mitano
ya umeme wa Upepo na Jua inajengwa Unguja na Pemba.
Amesema kuwa Jumuiya ya Umoja wa Nchi za
Ulaya (EU) imetoa jumla ya Uero milioni tatu kwa ajili ya kazi za awali
za ujenzi wa minara mitano Unguja na Pemba .
Mradi huo unajengwa kwa majaribio katika
maeneo ya wazi kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi utachukua miezi kumi
na nane ambayo ni sawa na mwaka mmoja na baada ya hapo ripoti ya wataalamu
kuwasilishwa serikalini.
No comments:
Post a Comment