Mgombea wake wa kiti cha ubunge kwa jimbo la Tanga Bw Musa Mbarouk akimwaga sera Jukwaani. |
Chama
cha Wananchi CUF leo kimezindua kampeni zake jijini Tanga kwa kumnadi mgombea
wake wa kiti cha ubunge kwa jimbo la Tanga Bw Musa Mbarouk kwenye viwanja vya
Tangamano jijini hapa.
Akizungumza na mamia ya wananchi
waliohudhuria mkutano huo Bwn Mussa ameahidi kuboresha Elimu, huduma za Afya sambamba
na Pato la mtu mmoja mmoja.
Amesema anauwezo,sifa na nia ya dhati ya
kuliongoza jimbo la Tanga hivyo anawaomba wakaazi wa Jimbo hilo wamchague kwa
kumpa kura za kutosha ili atimize ahadi anazoahidi.
Kampeni za vyama vya siasa nchini kuomba
ridhaa ya uongozi kwa wapigakura katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu
zimeanza kwa kasi jana kwa baadhi ya vyama husika kufungua kampeni zake kwa
vishindo huku vijembe na misemo ikitawala majukwa hayo.
No comments:
Post a Comment