WAANDISHI wa habari
Nchini wametakiwa kujiepusha kushabikia vyama vya siasa ili kuhakikisha
wanaandika habari zenye tija kwa jamii inayowazunguuka.
Rai
hiyo ilitolewa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe Hafsa Mtasiwa wakati ufunguzi wa
semina ya mafunzo kwa waandishi wa habari yaliyotolewa na mfuko wa taifa wa
bima ya afya NHIF yaliyofanyika wilayani humo.
Mkuu
wa wilaya huyo alisema nafasi ya mwandishi wa habari katika kufikisha habari
kwa jamii kwa kutumia kalamu zao ni kubwa hivyo ni vema kutoa habari za ukweli
bila ya kumuonea mtu ili amani ya nchi iweze kuendelea.
"Nafasi
yenu ni kubwa katika kuhabarisha jamii....lakini kalamu hiyo hiyo ikitumiwa
vibaya inaweza kuvuruga amani iliyopo ambayo tumeizoea"alisema Mkuu wa
wilaya huyo.
Hata
hivyo alitumia fursa hiyo kuwataka waandishi wa habari kuwakumbusha mara kwa
mara wananchi umuhimu wa kutunza kadi za kupigia kura ili baadae wakachague
viongozi watakao wataka.
"Ndugu
zangu waandishi wa kupitia vyombo vyenu vya habari naomba muwakumbushe wananchi
kutunza kadi zao ili siku ikifika wapate machaguo sahihi kusiwe na
lawama"alisema Hafsa.
Kwa
Upande wake Mkurugenzi wa mfuko wa afya CHF Eugen Mikongoti alisema lengo
ni kuhakikisha wanahabari wanakuwa na utaratibu wa kupata matibabu ili kuepuka
mazingira hatarishi.
"Kwa
kuelekea kwenye uchaguzi mkuu ni bora kila mwandishi apate kadi ya bima ya afya
ili kwani uwezi kujua pirika pirika zitakuwaje kulingana na wakati"alisema
Mkurugenzi Mkongoti.
No comments:
Post a Comment