HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Sunday, 16 August 2015

MFUKO WA NHIF WATOA MSAADA WA MASHUKA 520 KWA VITUO VYA AFYA WILAYANI YA MUHEZA.



Na Mariam Cypriam. TANGA
Mfuko wa Taifa wa bima ya afya mkoani hapa NHIF umekabidhi mashuka 520 yenye thamani sh 8,840,000kwa ajili ya matumizi katika wodi za kulaza wagonjwa kwenye vituo vya afya na zahanati kwa serikali wilayani muheza mkoani Tanga.

Makabdhiano hayo yalifanyika jana katika kituo cha afya cha Ubwari
mjini hapa kwa Meneja wa NHIF,Mkoa wa Tanga,Ali Mwakababu kumkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Muheza,Esterina Kilasi.

Akizungumza baada ya kupokea mashuka hayo,Mkuu wa Wilaya ya
Muheza,Esterina Kilasi aliishukuru NHIF kwa kuwa mstari wambele katika
kuboresha sekta ya afya Wilayani hapa na kuomba isichoke kusaidia
maeneo mengine.

"NHIF kwetu Muheza ni mdau muhimu katika sekta ya afya kwa sababu
tangu nimehamishiwa hapa hii ni mara ya pili sasa napokea misaada ya
mashuka kutoka mfuko huo tunaahidi kushirikiana nao hadi
kieleweke"alisema Kilasi.

Meneja wa NIHF Mkoa wa Tanga,Mwakababu alisema NHIF imetoa mashuka
hayo kufuatia ombi lililowasilishwa kwake na ofisi ya Mganga Mkuu wa
Wilaya ya Muheza likielezea uhaba wa mashuka katika wodi za ,vituo vya
afya na zahanati zilizopo Wilayani hapa.

"NHIF imeweza kutoa msaada huo ikitambua kwamba mashuka hayo
yatatumiwa na wadau wake lakini inawahamasisha kujiunga na mfuko huo
ili waweze kunufaika na matibabu hasa wanapougua"alisema Mwakababu.

Mganga Mkuu wa Wilayani hapa,Juma Mfanga alisema mashuka hayo
yatagawanywa katika wodi za kulaza wagonjwa zilizopo kwenye zahanati
33 pamoja na vituo vya afya vya Ubwari na Mkuzi.

Hata hivyo alisema Wilaya hiyo bado inakabiliwa na changamoto ya uhaba
wa vifaa tiba na kuiomba NHIF kuangalia eneo hilo kwani linachangia
kwa kiasi kikubwa kuzorotesha huduma za afya kwenye vituo vya afya na
zahanati.

No comments:

Post a Comment