Mkuu
Wa Wilaya Ya Tanga
Abdul
Lutavi
|
Imeelezwa kuwa kuporomokwa kwa maadili ya viongozi, ufisadi wa mali za ummma, matumizi mabaya ya madaraka pamoja na athari za utandawazi ikiwemo ukiukwaji wa haki za kibinadamu kuwa ni majanga yanayodumaza nguvu na uwezo vijana kujenga taifa lao.
Hayo yameelezwa na Afisa maendeleo msaidizi wa mipango miji, jijini Tanga, Vedastus Matagi wakati akisoma risala,kwa mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Tanga Abdul Lutavi, kwenye maadhimisho ya siku ya vijana yaliyofanyika uwanja wa tangamano hii leo.
Aidha amesema lengo lamaadhimisho hayo ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 12, mwezi Augost ni kutoa nafasi kwa jamii, hususan, kutafakari kwa kina juu ya matatizo na changamoto zinazokabili maisha ya vijana na kutafuta njia ya kuzipatia ufumbuzi wa kudumu.
Sambamba na hayo pia vijana mkoani hapa wameiomba serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, mifuko ya kijamii na wadau wote kwa ujumla, kuwa na mipango thabiti na shirikishi ili kuokoa maisha ya jamii haswa vijana.
Aidha kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Tanga ameahidi serikali kuhakikisha kuwa mipango inayowekwa kwasaidia vijana inawafikia, ili kuwaponya kwani wao ndio chanzo maendeleo ya taifa.
Siku hii maalum duniani ilianzishwa mwaka 1999, ambapo Tanzania ilianza kuadhimisha mwaka 2000.
No comments:
Post a Comment