Zaidi ya asilimia
23 ya watanzania wametajwa kuwepo katika hatari ya kupatwa na athari za
magonjwa yasiyoambukizwa ambayo huchangiwa na tabia hatarishi ikiwemo ulaji wa
vyakula vyenye mafuta uzito uliokithiri na kutokuwa na tabia ya kupima mara kwa mara.
Hayo yamesemwa na
Mkurugenzi wa taasisi inayojihusisha na upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza Dkt
Lwidiko Edward leo jijini Dar es salaam wakati wa kuhamasishaji kupima magonjwa
kama kisukari, presha, kiribatumbo ongezeko kubwa la watu haswa kundi la vijana
wanaoathiriwa na magonjwa hayo katika umri mdogo.
Dkt. Edward
ameongeza kuwa zaidi ya asilimia 8 ya wagonjwa wanaopimwa hawana ufahamu
kuhusiana na magonjwa yasiyoambukiza na kuwataka wanafamilia kujenga tabia ya
kupima afya mapema haswa kwa magonjwa yasiyoambukiza ambayo yamekuwa yakipuuzwa
huku yakiwa na athari kubwa miongoni mwa nguvu kazi katika jamii.
Kwa upande wake
mtaalamu na mshauri katika kampeni ya ijue afya yako bi Vanessa Chilunda
ameeleza kuwa gharama za kutibu magonjwa yasiyoambukiza ni kubwa sana ndio
maana wanafanya uhamasishaji haswa kwa vijana na wazazi kuweza kutambua umuhimu
wa kupima afya zao mara kwa mara pamoja na kujenga nidhamu katika ulaji wa
vyakula mbalimbali.
Chilunda amewataka
vijana kote nchini ambao ni kundi kubwa kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi
mara kwa mara na kuepuka maisha ya anasa ambayo huwaweka katika hatari kubwa ya
kupata magonjwa ya kisukari, presha, kiribatumbo na mengineyo yanayosababishwa
na ulaji mbovu wa chakula.
No comments:
Post a Comment