Na Mariam Cyprian,Tanga
Klabu ya African
Sport wana kimanumanu wamefanikiwa kufanya uchaguzi na kupata viongozi
watakaoiongoza klabu hiyo kwa kipindi kingine cha miaka minne ambapo wanaanza ukurasa
mpya wa wakishiriki mashindano ya ligi kuu ya soka Tanzania Bara msimu mpya wa
2015/16.
Akisoma matokeo
ya uchaguzi huo mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF Bw Aloyce Komba,alisema
klabu hiyo ilikuwa na wanachama 76 ambapo wanachama 52 ndio waliopiga kura
katika uchaguzi huo.Aidha
alimtaja Hassan Shehe kuwa ndie aliyeibuka kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo
akipita kwa kura zote zilizopigwa ambapo
katika nafasi hiyo hakuwa na mpinzani.
Alimtaja
Abdull Ahmed(Bosnia) kuwa ndie makamu mwenyekiti ambaye pia alipata kura zote
zilizopigwa huku akiwa hana mpinzani katika nafasi hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Uchaguzi ya TFF
Bw Aloyce Komba
|
Nafasi za
wajumbe zilikuwa tano ambapo wajumbe watatu walipatikana huku nafasi nyingine
mbili zikiachwa wazi baada ya Wajumbe wawili ambao ni Ally Ramadhani na Mohammed Omari kuondolewa
kwenye uchaguzi kutokana na sababu za kutokidhi vigezo vya kugombea.
Walioshinda
ni Mwinshame Mbwana aliyepata kura 52, Godios Kimath aliyepata kura 51 na
Abdallah Ahmed aliyejizolea kura 51 kati ya bkura zote zilizopigwa.
Akizungumza
baada ya uchaguzi huo Mkurugenzi Msaidizi wa Sheria na Uanachama kutoka TFF Bw Eliud
Mvella aliipongeza kamati ya uchaguzi ya African Sport kwa kuwa na maandalizi
mazuri yaliyofanikisha uchaguzi huo kufanyika kwa utulivu na amani sambamba na
tabia nzuri ya wanachama wa klabu hiyo kwa kuwa na maelewano baina yao.
Alisema
hakukuwa na usiri katika mchakato mzima wa wa uchaguzi huo kama inavyoelezwa na
baadhi ya watu kwani matangazo kuhusu uchaguzi huo yalitolewa mapema na kwa
uwazi.
Naye mwenyekiti
Hassan Shehe aliyechaguliwa ambaye pia ndiye aliyekuwa akiiongoza klubu hiyo
alisema atahakikisha anaiendesha vizuri klubu na kuwachukulia hatua wale wote
ambao watajaribu kuleta migogoro katika klubu hiyo.
No comments:
Post a Comment