Wito
umetolewa kwa wafanyabiashara nchini kuleta bidhaa zenye ubora ili kulinda afya
za watumiaji na kuepuka hasara pale zitakapokamatwa na shirika la viwango
nchini (tbs)
Wito huo umetolewa na Afisa masoko wa
shirika la Viwango Tanzania Gladness
Kaseka wakati akizungumza na kituo hiki kwenye maonesho ya wiki ya nenda kwa
usalama barabarani kitaifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Tangamano jijini
Tanga.
Amesema wanashiriki maonesho hayo kwa sababu
wao ni wadau wa mambo ya usalama na jukumu lao kubwa ni kusimamia viwango vya
bidhaa zote kitaifa akitolea mfano magari yanayoingizwa nchini ambayo hupimwa
kabla ya kuruhusiwa kuanza kutumika.
Kuhusu bidhaa za wajasiriamali wadogo wadogo
Bi Kaseka amesema kwa sasa Serikali imewapafursa ya kupata nembo ya ubora
kutoka tbs bure ili kuwawezesha kuuza bidhaa zao kwenye soko la ushindani
kitaifa na kimataifa.
Afisa huyo amebainisha kuwa ni wanajamii
wanapaswa kutoa taarifa juu ya bidhaa zisizo na ubora pindi wanapozibaini kupitia
namba ya bure ya 08110827 ili waweze kufanya ufuatiliaji na kuondosha bidhaa
hiyo sokoni.
Shirika la Viwango nchini (TBS) lina Ofisi
kwenye mipanga ya nchi bandari za Tanga na Dsm,uwanja wa ndege Dsm na sasa Serikali
imeongeza wafanyakazi 200 kwenye shirika hilo watakaowezesha utoaji wa huduma
kuenea kwenye mikoa ya Mbeya Arusha na Mwanza.
No comments:
Post a Comment