Jeshi
la Polisi kikosi cha Usalama barabarani nchini limeshauriwa kukagua vymbo vya
usafiri kisasa zaidi ili kubaini uwezo wake hasa injini za magari na pikipiki
ili kupunguza ajali zinazo sababishwa na ubovu na uchakavu wa vyombo hivyo.
Hayo yamesemwa na Afisa Masoko mwandamizi wa
kampuni ya Starpeco Co Ltd Bw Jones Mkoka wakati akizungumza na kituo hiki
kwenye maonesho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani kitaifa yanayoendelea
kwenye viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
Amesema kampuni hiyo inashiriki maonesho ili
kutoa elimu kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri vinavyotumia Oil juu ya matumizi
ya Oil sahihi sambamba na upimaji wa Oil kwa teknolojia ya kisasa ambayo ni
mpya nchini.
Afisa huyo amesema kupitia teknolijia hiyo
ya kupima Oil kwa kifaa maalum cha Computer mmiliki wa chombo cha usafiri
anaweza kubaini matatizo mbalimbali yaliyoko kwenye chombo chake, hivyo ni
wakati sasa shirika la viwango nchini
(tbs) kutumia teknolijia hiyo inapokagua ubora wa magari yanaliyotumika ambayo
huingizwa nchini kwa wingi.
Afisa Mkoka hakusita kuwakaribisha wakazi wa
mkoa wa tanga kwenye banda lao lililoko ndani ya viwanja vya maonesho kupata
elimu ya bure na pia kupima vyombo vyao vya usafiri kama magari na pikipiki kwa
gharama nafuu ambayo ni maalum kwa maonesho hayo.
No comments:
Post a Comment