Afisa Masoko,Usajili na Ukusanyaji wa mfuko wa hifadhi ya jamii wa GEPF Bw Eric Haule akiwa kwenye banda la mfuko huo ndani ya viwanja vya Tangamano jijini Tanga yanakoendelea maonesho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani kitaifa. |
Na Godwin Lyakurwa .TANGA.
Jamii imetakiwa kuwa
na utamaduni wa kujiwekea akiba kupitia mifuko ya hifadhi ya jamii itakayo
wasaidia pindi wanapokabiliwa na majanga mbalimbali kama ajali za barabarani
ambazo husababisha majeraha na ulemavu wa kudumu.
Hayo
yamesemwa na Afisa Masoko,Usajili na Ukusanyaji wa mfuko wa hifadhi ya jamii wa
GEPF Bw Eric Haule wakati akizungumza na kituo hiki kwenye banda la mfuko huo
katika maonesho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yanayoendelea kwenye
viwanja vya Tangamano jiji Tanga.
Amesema
ukweli ni kuwa hakuna mtu ajiuaye kesho yake kwani majanga ya ajali kuweza
kumkuta muda wowote hivyo akiba ni muhimu.
Afisa
huyo amesema wanashiriki maonesho hayo ili kutoa elimu kwa watumiaji wa
barabara juu ya kujiwekea akiba itakayosaidia baada ya kukumbwa na ajaili hivyo
kila mwananchi anakaribishwa kwenye banda lao lililoko ndani ya viwanja vya
maonesho hayo.
Mfuko
wa hifadhi ya Jamii wa GEPF unapokea wanachama wa hiyari na lazima ambao
hujiwekea akiba kwa mujibu wa sheria.
No comments:
Post a Comment