HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Tuesday, 4 August 2015

RAIS KIKWETE AFUNGUA WIKI YA NENDA KWA USALAMA NA KUWAAGA WAKAZI WA MKOA WA TANGA.




Rais Kikwete akiwasili kwenye viwanja vya Tangamano jana




Maandamano ya Wadau wa Usalama Barabarani








Rais Kikwete Jana amefungua maonesho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yanayofanyika kitaifa jijini Tanga.
Akihutubia mamia ya wananchi, viongozi wa jeshi la polisi, wasafirsihaji na wadau wanaojihusisha na kupiga vita ajali barabarani katika uzinduzi wa wiki ya nedna kwa usalama uliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga Rais Kikwete ameliagiza jeshi la polisi nchini kufanya kazi kwa uadilifu ikiwa ni pamoja na kuacha kupokea rushwa ili azma ya kukabiliana na ajali za barabarani zinazoendelea kupoteza maisha ya watanzania iweze kufikiwa.
Maadhimisho ya mwaka huu yamebebwa na ujumbe unaosema ''Endesha salama okoa maisha''

Naye mwenyekiti wa baraza la usalama barabarani nchini Mheshimiwa Pereira Slim amekemea wasafirishaji wanaoendelea kuvunja sheria na kuagiza kuwa sheria haitasita kuchukua mkondo wake kwa yeyote ambaye atakiuka sheria na taratibu zilizowekwa.
Hata hivyo Afisa mnadhimu wa makosa ya usalama barabarani nchini kamishna Johansen Kahatano amesema Asilimia 40% ya ajali za Barabarani zinazotokea kwa sababu ya makosa hatarishi zimedhibitiwa kufuatia wadau wa mbali mbali kuanzisha kampeni ya kuzuia ajali Barabarani.
Kamishna Kahataho mesema kuwa jitihada hizo zimesababisha katika kipindi cha miaka iwili iliyopita ajali za makosa hataraishi ikiwemo mwendo kasi ziepungua kwa asilimia 40% hatua ambayo imeonesha kuwa inaweza kuleta mafanikio na kupunguza vifo vya watanzania vitokanavyo na ajali.

Baada ya ufunguzi wa maonesho ya wiki ya nenda kwa usalama barabani Rais Kikwete alipata fursa ya kuwaaga wakazi wa mkoa wa tanga na kuiwashukuru kwa ushirikiano waliompatia kwa kipindi chote cha uongozi wake tangu mwaka 2005.

Amesema mafanikio makubwa yaliyopatikana ni juhudi za Serikali na wananchi hivyo ni jukumu la wananchi kuyendeleza hata baada ya kipindi chake kumalizika.

Rais kikwete hakusita kutoa angalizo kwa wakazi wa mkoa wa Tanga na wilaya yake juu ya kuendeleza Amani wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Naye mkuu wa mkoa wa Tanga Mh Said Magalula Said amemshukuru Rais Kikwete kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani hapa kama ujenzi wa barabara ya Tanga Horohoro na Mkata Handeni km 71.

Aidha Mkuu wa Mkoa amemuomba Rais Kikwete kumuagiza Rais ajaye kukamilisha ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani-Bagamoyo, kukuza bandari ya Tanga, kujenga Reli ya Tanga-Kilimanjaro itakayo unganisha mkoa wa Tanga na Mikoa ya Kanda ya Ziwa sambamba na kufufua viwanda vilivyokufa ili kinua uchumi wa mkoa watanga ambao utaboresha pato la mkazi mmoja mmoja.

No comments:

Post a Comment