BAADHI ya
wavuvi wa vijiji vya Ushongo na Stahabu wilayani Pangani Mkoani Tanga wanaiomba halmashauri
ya wilaya hiyo kuwapatia mafunzo maalum yatakayojengea stadi na uwezo wa
kuanzisha vikundikazi katika shughuli zao.
Wametoa ombi hilo kwenye hafla ya kufunga mafunzo
ya wiki moja kwa sekta isiyo rasmi kuhusu uvuvi endelevu, mafunzo yaliyoendeshwa
na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Kanda ya Kaskazini.
Ramadhani Seif mvuvi kutoka kijiji cha Stahabu amesema mafunzo aliyopata kuhusu uvuvi endelevu na ujasiriamali anaamini yatamletea tija zaidi endapo hasa halmashauri itawawesha wavuvi kuunda vikundi vya uzalishaji mali.

Pia Mwahija Silaha mvuvi wa kijiji cha Ushongo amesema
utekelezaji wa hatua hiyo utawakwamua ki uchumi kwa kuwezesha kufanya uvuvi
endelevu na hivyo kuondokana na hali duni ya maisha kwenye kaya.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa VETA Kanda ya
Kaskazini, Angelus Ngonyani amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha
kutambua sera na sheria za wavuvi na hatimaye kufanya shughuli zao kwa usahihi
na kujikwamua kiuchumi kwa kuongeza kipato katika jamii.
No comments:
Post a Comment