Hospitali
ya Mkoa Bombo kwa kushirikiana na Madaktari wa Shirika la Interplast la Ujerumani
inatazamia kutoa huduma ya bure ya
upasuaji wa kurekebisha maumbile kama kupasuka midomo ( cleft lips)
kupasuka kaakaa (cleft palate) Uvimbe ( turmors) na Makovu sugu ambayo
itakuwepo kwa muda wa siku 10.
Huduma ya upasuaji imeanza kwa uchunguzi wa wagonjwa
wenye matatizo hayo kisha kupangiwa tarehe ambapo uchunguzi wa awali unaanza tarehe
3/08/2015 zoezi litakalo dumu kwa majuma mawili.
Kwa mujibu wa mratibu wa zoezi hilo la upasuaji Dr
Wallace Karata, amesema ushirikiano wa upande hizi mbili katika kunusuru maisha
ya Watanzania ulianza mwaka 2011 ambapo
hospitali iliona umuhimu wa kuwasaidia wananchi hasa wale wasio na uwezo wa
kulipia upasuaji na matibabu.
Aidha, uandikishwaji wa wagonjwa wenye matatizo
mbalimbali unagharimu shillingi za kitanzania elfu tano (5000) na zaidi ya watu
150 wamejitokeza kufanyiwa uchunguzi wa awali kwa ajili ya upasuaji huo.
No comments:
Post a Comment