Mbwana Samatta ni mshambuliaji wa kimataifa kutokea Tanzania
anaeichezea klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo
ambayo alijiunga nayo mwaka 2011 akitokea Simba ya Tanzania na mpaka
sasa amekua mmoja kati ya wachezaji mahiri
wanaounda safu imara ya ushambuliaji kwa TP Mazembe na timu ya taifa ya Tanzania.
Samatta
aliingia kwenye headlines siku kadhaa zilizopita baada ya kukataa kusajiliwa na
klabu ya Zamalek ya Misri kwa euro milioni 1 kutoka TP Mazembe
ambayo ni sawa na zaidi ya bilioni 2.3 za Kitanzania, kila media
iliandika hii story nakuonekana kama Samatta
amepoteza bahati.
Wakala wa mchezaji huyo Jamal
Kasongo amezungumzia suala hilo na
mpango wa Samatta licha ya kupewa ofa ya
mshahara mkubwa.
La kwanza ni kweli
maafisa wa Zamalek wawili walifika kipindi mimi nipo na Mbwana kipindi yupo
katika mechi ya timu ya taifa kimsingi mimi niliweza kukaa nao chini kuweza
kufanya nao majadiliano lakini lazima mchezaji ili ufikie malengo uweze kukaa katika
mstari, msimamo wa Mbwana na msimamo wangu mimi kama mshauri wake ni Mbwana
kuweza kucheza Ulaya” alisema Jamal Kasongo
Wakatuma tena ofa wako tayari kumnunua TP
Mazembe kwa euro milioni 1 na euro milioni 1 ni pesa nyingi na walikuwa tayari
wakimuhitaji waweze kumpa mshahara ambao hakuna mchezaji ndani ya Afrika hii
anaweza akalipwa lakini bado hili suala lilikuwa gumu kwani lengo kubwa ni
Mbwana kucheza Ulaya” alisema Jamal Kasongo
Mbwana Samatta
anamaliza mkataba wake na TP Mazembe mwezi April 2016 hivyo anaweza kuwa
mchezaji huru na kuchagua timu ipi ya kwenda.
No comments:
Post a Comment