HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Wednesday, 29 July 2015

WAKULIMA WADOGO WA MKONGE MKOANI TANGA WASHAURIWA KUTUMIA KILIMO MSETO.



WAKULIMA wadogo wa mkonge mkoani Tanga wameshauriwa kutilia mkazo kilimo cha mazao mseto katika mashamba yao ili kujiongeza tija na kuinua uchumi.

Mratibu wa Utafiti wa Kilimo cha Mkonge wa Kituo cha Utafiti Mlingano, Shabani Hamisi kwamba utekelezaji wa mbinu hiyo ya kilimo unamwezesha mkulima kupunguza gharama za utunzaji shamba hasa katika kipindi cha miaka mitatu ya awali kabla ya kuanza kuvuna Mkonge.

Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanaendelea kutokea katika maeneo mbalimbali hapa nchini utafiti wetu sasa umebaini kwamba shughuli za kilimo mseto cha mkonge kwa kuchanganya na mahindi, kunde, ufuta au alizeti ndizo zinachoweza kumsaidia mkulima mdogo kuongeza tija kwenye uzalishaji.
Aidha ametaja faida nyingine ya Kilimo mseto ni kuongezea uhakika wa chakula kwenye kaya kwa kumsaida mkulima kuzalisha chakula wakati anaposubiri awamu ya kwanza ya kuvuna mkonge sambamba na kurutubisha udongo shambani.

Naye Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge, Yunus Msika amesema baadhi ya wakulima kutoka wilaya za Mkinga, Tanga, Muheza na Korogwe wana  lengo moja la  kuwashawishi wakulima kutumia fursa hiyo kuongeza uzalishaji utakaowapatia mavuno mengi ya aina mbalimbali katika eneo dogo.

Kwa upande wao baadhi ya wakuliwa akiwemo Abdi Shekighenda wa Mwelya kilimo mseto msimu huu kimempa uwezo wa kumudu kusafisha shamba lake ambalo awali lilikuwa pori na kusababisha mkonge kudhoofika.

No comments:

Post a Comment