MKUU
wa Mkoa wa Tanga, Said Magalulla, ameyataka makampuni ya simu nchini kupunguza
gharama za matumizi ya simu ili kuwawezesha watu wa kipato cha chini kuweza
kumudu matumizi ya mitandao hiyo.
Akizungumza mara baada ya kufungua
kituo cha huduma kwa wateja cha kampuni ya simu ya Airtel mjini hapa
jana, Magalulla alisema gharama za matumizi ya simu ziko juu hivyo ni
wajibu wa makampuni hayo nchini kumuangalia mtu wa kipato cha chini.
Alisema asilimia kubwa ya watumiaji wa
simu ni watu wa kipato cha chini jambo ambalo limekuwa kikwazo kwa
maendeleo ya jamii na kuzidisha ugumu wa maisha.
“Mawasiliano ya simu nchini yanazidi
kukua kwa kasi ila changamoto iko katika gharama za matumizi tumeona
gharama zikiongezeka lakini hatuoni zikipungua” alisema Magalula na kuongeza
“Hebu nyinyi airtel tuliopo hapa
onyesheni mfano kwa wengine ili kuiga kutoka kwenu kufungua kituo
kikubwa cha huduma kwa wateja hapa kwetu ni wazi kuwa pato kubwa linatoka
kwa mtumiaji tena wa kipato cha chini” alisema
Alisema kituo hicho kitakuwa msaada
mkubwa kwa wananchi wa Tanga na watumiaji wa mtandao wa Airtel na hivyo kuitaka
kuboresha huduma zake zikiwemo za watumiaji wa intareti na simu.
Wakati huo huo Mkurugenzi wa
huduma kwa wateja Tanzania, Adriana Liamba, alisema malengo ya kampuni ya simu
ya Airtel ni kumfikia kila mmoja wa mjini na vijijini na hivyo kuwa na mipango
ya kupeleka huduma hiyo kila pembe.
Alisema mbali ya changamoto kampuni ya
simu inayokumbana nayo lakini imeweza kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali
zikiwemo za kujenga majengo ya shule na zahanati pamoja na vifaa vya elimu kwa
wanafunzi mashuleni.
“Kampuni inakabiliwa na changamoto
mbalimbali kuhakikisha kila mtu inamfikia huduma ya mtandao katika eneo
alilo----ikumbukwe kuwa tumefanya mengi mazuri yakiwemo kujenga majengo ya
shule na vituo vya afya” alisema Liamba
Ameitaka jamii kushirikiana na kampuni
ya Airtel ili kuweza kurahisha maendeleo na ustawi wa uchumi wa nchi na kila mmoja
kufaidika na huduma hiyo muhimu kwa jamii.
No comments:
Post a Comment