HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Thursday, 21 May 2015

MADAWA YA KULEVYA YAKAMATWA TARAFA YA PONGWE JIJINI TANGA



JESHI la polisi mkoa wa Tanga linamshikilia Omari Mganga mewnye umri wa miaka28 mkazi wa Mapinduzi kwa kumkuta na madawa ya kulevya  kete kumi na tatu ambayo aina na dhamani yake bado haija fahamika

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Zuberi Mombeji amesema mnamo may 20 huko maeneo ya Tangasisi Tarafa ya Pongwe Polisi  walimkamata Mganga akiwa na  madawa hayo na pia mtuhumiwa ni muuzaji wa madawa hayo ya kulevya.

Katika tukio linalofanana na hilo Jeshi la Polisi linamshikilia  Nasimu Hasani mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa barabara ya nane Tanga Mjini kwa kukutwa na mirungi kilo kumi na tano.
Akidhibitisha tukio hilo kamanda Mombeji amesema may 19 majira ya saa tano asubuhi huko kabuki polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa anayasafirisha madawa hayo kwenye gari lenye namba za usajili T 836 CHF mali ya Kampuni ya Ratco.

No comments:

Post a Comment