Kikosi cha Coffee fc |
Ligi ya Hamasa Cup imeendelea leo kwa
Mchezo mmoja mkali ambapo Home Guard Fc walipambana na Coffee fc katika Dimba
za Ziwani kata ya Pongwe jijini Tanga.
Katika mchezo
huo timu ya Home Guard imeendeleza ubabe mbele ya vijana wa Cofee kwa kuwachapa
bao 1-0, mchezo uliojaza mashabiki wengi kutoka maeneo mbalimbali ya jiji
kutokana na mvuto wa historian na mahusiano ya timu zote mbili.

Kama kawaida
Coffee fc imeendela kucheza soka lake la
pasi nyingi na kasi lakini bado tatizo la umakini na upangaji mzuri wa
mashambilizi ni kikwazo kwa timu hiyo kupata ushindi.
Ligi hiyo
itaendela kesho kwa mchezo mmoja utakaopigwa katika uwaja huohuo ambapo Middle
Age watapambana na Bamba Ngumu fc.
Mchezo wa jana Young Rovers waliiburuza timu ya Pongwe Shooting bao 6-2 kikiwa ni kipigo kikubwa zaidi kweye ligi hiyo mpaka sasa.
Mchezo wa jana Young Rovers waliiburuza timu ya Pongwe Shooting bao 6-2 kikiwa ni kipigo kikubwa zaidi kweye ligi hiyo mpaka sasa.
No comments:
Post a Comment