Zoezi la kuandikisha vitambulisho vya
Uraia linaendela kwenyevituo vya kata ya Pongwe ambapo wananchi wengi
wanaendela kujitokeza kwa wingi kutimiza haki yao ya msingi.
Kituo cha Pongwe kaskazini kimekuwa na msongamano mkuibwa wa watu kulinganisha na vituo vingine ambapo kinamama na vijana wamekuwa wakitumia zaidi ya masaa saba kusubiri huduma hiyo hali inayoonesha jinsi gani zoezi hili limepokelewa vizuri na wananchi.
Akizungumza
na mtandao huu Afisa Mtendaji wa kata ya Pongwe Bw Sali Mdoe amesema zoezi hilo
linaendela vizuri kwani mashine zimegawanywa kwa kituo cha Pongwe kaskazini ili
kurahisisha kazi kwa watendaji huku akipongeza wananchi kwa kujitokeza kwa
wingi kweny vituo hivyo.
![]() |
Mr Method Kapinga. |
Mtandao huu
umefanya mahojiano na baadhi ya wananchi waliofika kwenye kituo cha Pongwe
kaskazini ambao wamekuwa na maoni tofauti juu ya zoezi hilo.
![]() |
Mr Moses Gasper |
“Zoezi
linaendela vizuri hakuna shida yoyote sisi Wazee tunahudumiwa kwa utaratibu
tofauti na vijana jambao ambalo ni zuri na linaondoa usumbufu kwenye kituo hiki”
Alisema mzee mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mr Method Kapinga.
“Kwa upande
wangu sijaridhishwa kabisa na mwenendo wa zoezi hili, nimefika hapa tangu saa
12 asubuhi na sasa ni saa saba mchana bado sijapata haki yangu ya kuandikisha,
mimi nimejiajiri mwenyewe sasa muda wote huu niko hapa kazi nitafanya saa
ngapi? Alisema mwananchi mwingin alijitambulisha kwa jina la Moses Gasper.
Moses
alimalizia kwa kuitaka Serikali kuthamini muda wa wananchi wake ambao wengi
hawana ajira kwa kufanya maandalizi ya kutosha kabla ya kuendesha zoezi kama
hili ambapo ni muhimu kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment