Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni toka Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Hermas Mwansoko akimkabidhi Afisa
Ustawi wa Jamii anayesimamia kituo hicho cha wazee Bi Otilia Daniel fedha za
kununulia mahitaji mengine wakati wa ziara ya kutoa msaada katika kituo hicho jana
Mkoani Tanga.
|
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah
Mwambene,Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania
Innocent Mungy (mwenyeshati la mistari) na Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni
toka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Hermas Mwansoko
(katikati) wakimkabidhi kiroba cha mchele moja ya Wazee wa Kituo
cha Mwanzange Mkoani Tanga, ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na Maafisa
Habari na Mawasiliano wa Serikali katika kikao kazi kinachoendelea Mkoani hapa.
|
Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wazee wa kito cha Mwanzange ambapo walitoa
Unga sembe Kilo 200,mchele kilo 300,mafuta ya kupikia dumu 2,mafuta ya
kupaka,dawa za meno,chumvi,sukari,maharage,nyama,majani ya chai,kanzu,misuli
pamoja na nguo za kinamama.
|
No comments:
Post a Comment