Mkuu wa Mkoa na Timu yake |
Afisa Mtendaji wa Kata ya Pongwe Salimu Mdoe akisoma taarifa ya Kata |
Kutoka Kushoto Diwani wa Kata ya Pongwe Bi Mwana Uzia,Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Omar Guledi,Mkuu wa Wilaya ya Tanga Bi Halima Dendego na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Luteni Mstaafu Chiku Gallawa |
Wakaazi wa Pongwe |
Mkuu wa Mkoa akizungumza na Wananchi |
Wananchi wa Kata ya Pongwe |
Wanafunzi wa Pongwe Sekondari |
Watendaji wa Kata wakijitetea kwa Mkuu wa Mkoa Meya wa Jiji |
Mkuu wa Mkoa Luteni Mstaafu Chiku Gallawa akiweka jiwe la Msingi katika Chumba cha Maabara Shuleni hapo |
Na Godwin Lyakurwa Tanga
Mnamo Feb 03 mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Luteni Mstaafu Chiku Galawa alifanya ziara kwenye kata mbalimbali jijini Tanga kwa lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleom kwa wananchi na kupokea taarifa za Uwajibikaji wa Watendaji wa hao.
Kituo cha kwanza katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa kilikuwa ni kata ya Pongwe ambapo alibaini Uzembe kwa watendaji wa kata hiyo,walioshindwa kusimamia ujenzi wa maabara 3 kwa shule ya Sekondari ya Pongwe na kufanikisha Ujenzi wa Chumba kimoja tu cha maabara tena kwa kutegemea Fedha za wahisani pasipo kukusanya michango ya wananchi.
Mh Luteni Mstaafu Chiku Gallawa alilazimika kutoa angalizo la kuongeza kasi ya Uwajibikaji kwa watendaji hao baaada ya kutaka kuona kitalu cha miti katika shule hiyo ambapo Mwl Mkuu wa Shule hiyo Mr Kamtoi alishindwa kumuonesha kitalu hicho.
Pia Mwalimu alishindwa kutoa majibu ya kuridhisha kwa mkuu wa Mkoa kufuatia kumuuliza kuhusu Amri ya Serikali kutaka shule kuwa na Uzio wa Mkonge.
Mkuu wa Mkoa alimbana Mwalimu huyo kwa maswali ambapo Mratibu Elimu wa Kata hiyo Bi Dora alilazimika kuingilia kati akijaribu kuokoa Jahazi ambapo nae alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kueleza kuwa wanazo mbegu za miti na Ndipo Mkuu wa Mkoa akahitaji kuziona lakini ikashindikana.
Kufuatia hali hiyo mkuu wa Mkoa amewataka watendaji wa Kata hiyo (Wakiongozwa na Afisa Mtendaji Ndg Salimu Mdoe )kuwajibika na kurekebisha makosa hayo haraka iwezekanavyo na kuwasilisha taarifa ya Utendaji Oficini kwake.
No comments:
Post a Comment