Wilaya 31 nchini zimegundulika kuwa na
madini ya aina mbalimbali kutokana na utafiti uliofanywa na Wakala wa Jiolojia
nchini (GST) kwa kushirikiana na Wizara ya Madini.
Utafiti huo ulifanywa kwa kutumia vifaa
vya kisasa kama ndege kwa ajili ya kupima ramani kwenye maeneo yenye
madini.
Hayo yalibainishwa katika kongamano la
uzinduzi wa taarifa za utafiti wa Fizikia ya Miamba (Jiofizikia) uliofanyika
katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini
Dar es Salaam, juzi.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo |
“Tunachokifanya hapa, ni kujua kiasi
gani cha madini yaliyopo nchini. Huu ni mradi mkubwa sana, tulitumia teknolojia
ya kisasa kwa kutumia ndege angani, tofauti na tafiti zilizokuwa zinafanywa
miaka ya 70,” alisema Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo wakati akizindua taarifa hizo.
Kwa mujibu wa Profesa Muhongo, mradi
huo ni wa mara ya kwanza kutumia vyombo vya kisasa kujua madini yaliyopo chini
ya ardhi ya Tanzania, ulihusisha wilaya 31 ambazo ziligundulika kuwa na madini
ya aina mbalimbali.
Alitaja wilaya hizo kuwa ni pamoja na
Dodoma, Bahi, Chamwino, Kongwa, Mpwapwa, Kondoa, Manyoni, Ikungi, Singida, Mkalama,
Iramba, Igunga, Kiteto, Hanang na Babati.
Nyingine ni Simanjiro, Mbulu, Arumeru, Monduli,
Moshi, Handeni.Kilindi, Korogwe, Chemba, Mvomero, Kilosa, Gairo,
Bagamoyo, Chunya, Mbozi na Mbarali.
No comments:
Post a Comment