CHELSEA YARUHUSU MATA KUPIMWA AFYA MAN UNITED!
>>NI BAADA KUKAMILISHA DILI YAO NA MMISRI MOHAMED SALAH!>>MATA KUPIMWA AFYA OLD TRAFFORD USIKU HUU!!
INGAWA Manchester United na Chelsea zilishakubaliana Ada ya Uhamisho ya Pauni Milioni 37 kwa Juan Mata kuhama, Chelsea walikuwa wamezuia Kiungo huyo wa Spain kukamilisha Dili hiyo hadi wao wamefikia Makubaliano na FC Basel ya Uswisi kuhusu kumnunua Mohamed Salah.
Jioni hii, Chelsea imethibitisha Dili ya kumnunua Salah imekamilika na imedokezwa kuwa sasa Mata ameruhusiwa kwenda Manchester kupimwa Afya yake Usiku huu.
Tangu Mchana, kuna Helikopta iliwekwa tayari kumrusha Mata kwenda kupimwa Afya.
Tayari Mata, mwenye Miaka 25, alishaafikiana na Man United Mkataba wa Miaka 4 ½ na Mshahara wa Pauni 150,000 kwa Wiki na Uhamisho wake utatangazwa Rasmi wakati wowote sasa.
Mechi ya kwanza kwa Mata akiwa na Man United inaweza kuwa Jumanne ijayo wakati Cardiff City watakapotua Old Trafford kucheza Mechi ya Ligi Kuu England.
Mata, ambae ameichezea Spain mara 32, alijiunga na Chelsea Mwaka 2011 alipohamia kutoka Valencia ya Spain.
Ikiwa Dili hii itakamilika, basi itavunja Rekodi ya Man United ya kununua Mchezaji kwa Bei ghali ambayo iliwekwa Septemba 2008 walipomnunua Dimitar Berbatov kutoka Tottenham kwa Pauni Milioni 30.75.
WASIFU:
Jina: Juan Manuel Mata GarcĂa
Kuzaliwa: 28 Aprili 1988 (Miaka 25)
Namba ya Jezi: 10
Timu za Vijana
1998–2003 Real Oviedo
2003–2006 Real Madrid
Timu za Kwanza
[Magoli kweye Ligi tu]
2006–2007 Real Madrid B Mechi 39 Goli 10
2007–2011 Valencia Mechi 129 Goli 33
2011– Chelsea Mechi 82 Goli 18
Timu ya Taifa
2004 Spain U16 Mechi 3 Goli 2
2004 Spain U17 Mechi 2 Goli 1
2006–2007 Spain U19 Mechi 13 Goli 12
2007 Spain U20 Mechi 5 Goli 3
2007–2011 Spain U21 Mechi 19 Goli 5
2012 Spain U23 Mechi 4
2009– Spain Mechi 32 Goli 9
+++++++++++++++++++++++++++
No comments:
Post a Comment