SKANDALI NEYMAR AZUA BALAA BARCA RAIS WA AKLABU HIYO SANDRO ROSELL AJIUZULU!
>>NI
KUFUATIA KUTINGA MAHAKAMANI WAKICHUNGUZWA UBADHIRIFU UHAMISHO WA NEYMAR!
ZIMEIBUKA
ripoti huko Spain kuwa Rais wa FC Barcelona, Sandro Rosell, amewasilisha uamuzi
wake wa kujiuzulu wadhifa wake.
Inadaiwa
Rosell alilipua uamuzi huo wakati alipotembelewa na Josep Maria Bartomeu na
Javier Faus, ambao wote wawili ni Makamu wa Rais wa Barca.
Hata
hivyo, Usiku huu kipo Kikao cha Dharura cha Bodi ya Klabu ambacho kitajadili
nini mustakabali wa Klabu kufuatia kutinga Mahakamani wakichunguzwa kwa
Ubadhirifu wa Fedha kwenye Uhamisho wa Supastaa wa Brazil Neymar kutoka Santos
kwenda Barca mwanzoni mwa Msimu.
Tuhuma
dhidi ya Barca na Rosell ni gharama halisi za Uhamisho wa Neymar ambao Barca
walitangaza kuwa ni Uhamisho wa Dau la Euro Milioni 57.1 wakati yapo madai ni
zaidi ya hapo na yapo malipo ya siri yaliyofanyika.
Kesi
hii, itasikilizwa na Jaji Pablo Ruz ambae anatarajiwa kukusanya taarifa toka
kwa Neymar, Santos na Barcelona kabla hajamwita Rosell aende mwenyewe
Mahakamani kutoa Ushahidi.
Kesi
hii inafuatia malamiko ya Mwanachama wa Barcelona, Jordi Cases, ambae ameungwa
mkono na Waendesha Mashitaka wa Spain waliokubaliana na Madai yake kwamba
kulikuwepo ubadhirifu na ukiukwaji wa Sheria kwa kutumia Mkataba Feki.
Pia,
wametaja Kitita cha Euro Milioni 40 kilicholipwa kwa Kampuni ya Baba yake
Neymar ambacho hakikutangazwa katika Uhamisho huo.
Juzi
Jumatatu, Gazeti maarufu huko Spain, El
Mundo, lilitoboa kuwa Dau halisi la kumnunua Neymar ni Euro
Milioni 95 kitu ambacho kilimfanya Rais Sandro Rosell atake nafasi Mahakamani
ili atoe ushahidi na kujisafisha.
Hiyo
Jumatatu, Rosell, akiongea na Wanahabari alitamka: “Kuna vitu viwili nataka
kusema. Kwanza Neymar aligharimu Euro Milioni 57.1. Na hili nimesema mara
nyingi. La pili, ni ombi, kwa heshima namuomba Jaji aniite ili nitoe ushahidi
na kumwambia kila kitu anachotaka kujua kwa sababu hamna cha kuficha!”
Katika
kuisikiliza Kesi hii, Jaji Pablo Ruz anatarajiwa kukusanya taarifa toka kwa
Neymar, Santos na Barcelona kabla hajamwita Rosell aende mwenyewe Mahakamani
kutoa Ushahidi.
Rosell
alishinda Uchaguzi wa Rais wa Barca Mwaka 2010 na alitakiwa ashike wadhifa huo
hadi 2016 lakini sasa Nafasi hiyo itakamatwa na Bartomeu hadi Uchaguzi ujao.
No comments:
Post a Comment