MKE
WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE
|
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
amewataka Watanzania kuongeza juhudi za kuzuia maambukizi ya Virusi
Vya Ukimwi(VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa
mtoto ili katika Tanzania iweze kuwa na kizazi kisichokuwa na VVU
na ugonjwa wa Ukimwi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mama Kikwete
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA)
wakati akifungua mkutano wa kitaifa wa wadau wa kuzuia maambukizi ya VVU
kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Aidha mama Kikwete aliwataka Watanzania kuchangia
sh. 100 katika kupambana na tatizo kwa mchango utawapa nguvu wadau
wengine kuwaunga mkono.
Aliwataka wadau wamaendeleo kuendele kuunga
mkno katika juhudi za kuondokana na tatizo hilo.
“ Lazima juhudi za makusudi zifanyike bila
kuchoka kwa maeneo yote Serikali, NGO’s, taasisi za dini mashirika ya kiraia na
watu binafsi . Hii itasaidia kunusuru kizazi chetu na kuwa na nguvu kazi
iliyobora, kizazi kisichokuwa na maambukizi na VVU na Ukimwi,” alisema Mama
Kikwete huku akisisitiza Tanzania bila Ukimwi inawezekana.
Aliongeza kuwa mikakati imara na endelevu ni
lazima iwepo kama vile kutoa huduma za kuzuia maambukizi ya VVU na Ukimwi kwa
kushirikisha jamii na kutoa tiba kikamilifu zinaweza kupunguza maambukizi hayo.
Alisema asilimia 98 ya wakina mama
wajawazito wanahudhuria kiliniki angalau mara moja na asilimia 43 mara
nne wakati wa ujauzito kati ya hao, asilimia 81 wanapimwa VVU.
Aliwataka wakina mama wajazito kuhudhuria kiliniki
wakati wa ujauzito kuanzia siku ya kwanza hadi watakapoajifungua
ili idadi ya wanahudhuria kiliniki iweze kufikia asilimia 100.
Naye Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.
Seif Rashid alisema hivi sasa Tanzania imefanikiwa kupunguza maambukizi hayo kwa
asilimia 15 mwaka 2012 kutoka asilimia 19 mwaka 2011 na
lengo ni kufikia asilimia 5 ifikapo mwaka 2015.
Alisema asilimia 90 ya wakina mama wajawazito
wamepimwa VVU kati yao asilimia 64 wamegundulika wanaishi na VVU , pia asilimia
55 ya watoto wanapatiwa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo.(ARV’s).
Kaimu Mkurugenzi wa Kinga kutoka wizara hiyo ,
Dk .Neema Rusibamayilla alisema alisema awamu ya pili ya kupambana
na tatizo hilo itaanza Januari mwaka huu katika mikoa mingine 16.
Mratibu wa huduma hiyo kutoka Malawi, Dk.
Michael Eliya alisema ni muhimu kuweza katika utoaji wa huduma,
kuboresha miundombinu ,ikiwemo rasilimali fedha na watu katika kufanikisha
malengo hayo.
No comments:
Post a Comment