Ø Jkt Oljoro kutua
Tanga ikiwa chini ya Kocha wa zamani wa Coast Hemed Morocco
Mzunguko
wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza
Jumamosi (Januari 26 mwaka huu) kwa mechi tano katika miji ya Bukoba, Dar es
Salaam, Tanga wakati mechi ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting inahamishiwa
uwanja mwingine.
Ashanti
United itacheza na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Coastal Union itacheza na
Oljoro JKT katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wakati Uwanja wa Azam Complex, Dar
es Salaam utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Azam na Mtibwa Sugar.
Jumapili
(Januari 26 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya JKT Ruvu na Mgambo Shooting
itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex wakati Simba na Rhino Rangers zitaumana
kwenye Uwanja wa Taifa.
Mechi
ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting iliyokuwa ichezwe Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sokoine inahamishiwa uwanja mwingine kwa vile huo bado nyazi zake ambazo
zimepangwa hivi karibuni hazijawa tayari kuhimili mechi hiyo.
KOCHA WA JKT OLJORO HEMED MOROCCO(Picha
kwa hisani ya Bin Zubeiry)
|
Hivyo
Tanzania Prisons inatakiwa kutafuta uwanja mwingine unaokidhi viwango
vinavyotakiwa kwa ajili ya mechi hiyo, na nyingine dhidi ya JKT Ruvu
itakayochezwa Januari 29 mwaka huu.
Pia
matumizi ya tiketi za elektroniki yanaanza katika mzunguko huu kwa vile viwanja
nane ambavyo tayari vimefungwa vifaa vya tiketi hizo. Vilevile tunakumbusha
washabiki wa mpira wa miguu kuwa tiketi za elektroniki haziuzwi viwanjani.
TWIGA STARS
|
TWIGA
STARS KUIVAA ZAMBIA FEB 15 LUSAKA
Tanzania
(Twiga Stars) itaivaa Zambia katika mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza ya
michuano ya mchujo ya Afrika kwa Wanawake (AWC) itakayofanyika Februari 15
mwaka huu jijini Lusaka.
Mechi
hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Nkoloma kuanzia saa 9 kamili kwa saa za Zambia
na itachezeshwa na mwamuzi Salma Mukansanga kutoka Rwanda.
Mukansanga
atasaidiwa na Wanyarwanda wenzake; Francine Ingabire, Sandrine Murangwa na
Angelique Tuyishime. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Jackey Gertse kutoka
Namibia.
KISHONGOLE,
KESSY KUSIMAMIA MECHI ZA CAF
Shrikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua Watanzania Alfred Rwiza Kishongole na
Lina Kessy kuwa makamishna wa mechi za shirikisho hilo zitakazochezwa wikiendi
ya Februari 14 mwaka huu.
Kishongole
ameteuliwa kusimamia mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Cote d’Or ya
Shelisheli na Kabuscorp de Palanca ya Angola.
Mechi
hiyo ya marudiano ya raundi ya mchujo itafanyika Shelisheli na itachezeshwa na
waamuzi kutoka Madagascar wakiongozwa na Abdoul Ohabee Kanoso. Waamuzi wengine
ni Basile Alain Rambeloson, Augustin Gabriel Herinirina na Andofetra Avombitana
Rakotojaona.
Naye
Kessy atakuwa kamishna wa mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza ya Kombe la
Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Rwanda na Kenya itakayochezwa jijini Kigali.
Waamuzi
wa mechi hiyo wanatoka Cameroon. Mwamuzi wa kati ni Sylvie Abou wakati
wasaidizi wake ni Winnie li Koudangbe, Lum Rochelle na Jeanne Ekoumou.
Boniface
Wambura Mgoyo
Ofisa
Habari na Mawasiliano
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
LIGI
KUU VODACOM
MSIMAMO:
NO
|
TEAMS
|
P
|
W
|
D
|
L
|
GF
|
GA
|
GD
|
PTS
|
1
|
Young
Africans
|
13
|
8
|
4
|
1
|
31
|
11
|
20
|
28
|
2
|
Azam
FC
|
13
|
7
|
6
|
0
|
23
|
10
|
13
|
27
|
3
|
Mbeya
City
|
13
|
7
|
6
|
0
|
20
|
11
|
9
|
27
|
4
|
Simba
SC
|
13
|
6
|
6
|
1
|
26
|
13
|
13
|
24
|
5
|
Kagera
Sugar
|
13
|
5
|
5
|
3
|
15
|
10
|
3
|
20
|
6
|
Mtibwa
Sugar
|
13
|
5
|
5
|
3
|
19
|
17
|
2
|
20
|
7
|
Ruvu
Shootings
|
13
|
4
|
5
|
4
|
15
|
15
|
0
|
17
|
8
|
Coastal
Union
|
13
|
3
|
7
|
3
|
10
|
7
|
3
|
16
|
9
|
JKT
Ruvu
|
13
|
5
|
0
|
8
|
10
|
16
|
-6
|
15
|
10
|
Rhino
Rangers
|
12
|
2
|
4
|
6
|
9
|
16
|
-7
|
10
|
11
|
JKT
Oljoro
|
13
|
2
|
4
|
7
|
9
|
19
|
-10
|
10
|
12
|
Ashanti
United
|
13
|
2
|
4
|
7
|
12
|
24
|
-12
|
10
|
13
|
Tanzania
Prisons
|
12
|
1
|
5
|
6
|
6
|
16
|
-10
|
8
|
14
|
Mgambo
JKT
|
13
|
1
|
3
|
9
|
3
|
23
|
-20
|
6
|
RATIBA
RAUNDI
YA PILI
Jumamosi,
25 Januari 2014
Ashanti
United v Yanga
Azam
FC v Mtibwa Sugar
Coastal
Union v JKT Oljoro
Kagera
Sugar v Mbeya City
Jumapili,
26 Januari 2014
JKT
Ruvu v Mgambo JKT
Simba
v Rhino Rangers
Tanzania
Prisons v Ruvu Shootings [Imeahirishwa, Sababu ya Uwanja]
No comments:
Post a Comment