KING CLASS MAWE |
BONDIA bora wa mwaka 2013,2014 katika uzito wa KG
63 Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ ame saini mkataba wa kupambana na
Cosmas Cheka Feb 8 mwaka huu katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam.
Mara baada ya kusaini mkataba huo wa kucheza raundi 10 za
ubingwa wa Taifa kg,60 amesema atafanya mazoezi ya kutosha kuhakikisha ana
msambalatisha mpinzani wake raundi za awali kwa kuwa alikuwa anachonga sana juu
yake .mpambano huo uliodhaminiwa na Promota Maarufu nchini Jay Msangi utakuwa
na msisimko wa aina yake kutokana na mabondia hawo kuwa gumzo katika ulimwengu
wa masumbwi ndani na nje ya nchi ya tanzania
King Class aliongeza kwa kusema kuwa nipo fiti
nimejiandaa na ninasubili tu kuvishwa ubingwa huo wa taifa kwani Cheka ana
ujanja kwangu mbinu zake zote nimesha zikamata
King Class Mawe anae nolewa na jopo la makocha wanao
ongozwa na Habibu Kinyogoli ‘Masta’ Rajabu Mhamila ‘Super D’ Kondo Nasoro
Bondio huyo amewashukulu wadau wa mchezo wa ngumi kwa kumuwezesha
kuchaguliwa kuwa bondia bora wa mwaka katika uzito wake kwa kuwapita mabondia
wengine wanne na yeye kuibuka kidedea katika kin’yan’gan’yiro hicho
No comments:
Post a Comment