UCHAGUZI Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
(TASWA), utafanyika Februari 16 mwaka huu jijini Dar es Salaam kama
ulivyopangwa na Kamati ya Utendaji ya chama.
Hata hivyo sekretarieti ya TASWA imekubaliana kusogeza mbele muda wa
kulipia ada kwa wanachama hadi Jumanne Februari 4 mwaka huu, badala ya Ijumaa
Januari 31, 2014 iliyokuwa imepangwa awali, lengo likiwa ni kuwezesha wanachama
wengi zaidi kulipia ada zao ili waweze kushiriki uchaguzi huo.
Wanachama wote walioshiriki uchaguzi wa mwaka 2007 ama 2010 au Mkutano
Mkuu wa mwaka 2012 wana sifa ya kushiriki uchaguzi huo wanachotakiwa kufanya ni
kulipia ada zao kuanzia mwaka 2011.
Malipo yafanywe kwa Mhazini Msaidizi, Mohammed Mkangara, 0658-123082 na
hakuna mwanachama mpya atakayekubaliwa kujiunga na chama kwa sasa mpaka baada
ya Uchaguzi Mkuu.
Nawasisitiza wanachama kuhakikisha wanatumia vizuri muda uliobaki kwa
kulipia ada zao ili waweze kushiriki mkutano huo. Kamati ya Uchaguzi ya TASWA
inatarajiwa kukutana Jumatatu ijayo kuzungumzia mambo mbalimbali yahusiyo
uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment