![]() |
‘Cannavaro’ |
Nahodha na beki
wa kati wa Taifa Stars, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ametangaza rasmi kuwa, atastaafu
kuichezea timu hiyo miaka mitatu ijayo.Kauli huyo, aliitoa
jana Alhamisi mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu yake ya Yanga kwenye
Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar.
Mara baada ya Stars kufungwa na Algeria mabao 7-0, kuliibuka
maneno kuwa Cannavaro na beki mwenzake wa kati, Kelvin Yondani, wanaonekana
kuchoka kutokana na umri kuwatupa mkono.
Cannavaro ameliambia gazeti hili kuwa umri wake siyo mkubwa
kiasi cha yeye kustaafu kuichezea Stars.
“Hizo kejeli na maneno ya watu nimeyazoea muda mrefu sana,
kuhusiana na kiwango changu kushuka na umri kuwa mkubwa, hivyo ninachofanya ni
kunyamaza tu.
TAMBWE AONGEZA MAJERUHI JANGWANI.
WAKATI kikosi cha Yanga kinatarajia
kuingia kambini Jumatatu ijayo kujiandaa na michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania
Bara itakayofanyika mkoani Tanga, mshambuliaji Amis Tambwe ameshindwa kuanza
mazoezi kutokana na maumivu ya shingo.
Yanga
itacheza mchezo wa raundi ya 10 dhidi ya Mgambo Shooting Desemba 12 mwaka huu
Uwanja wa Mkwakwani Tanga, kisha siku chache baadaye itacheza na African Sports
kwenye uwanja huohuo.
Akizungumza
na gazeti hili jana, Kocha Mkuu wa Yanga Hans Pluijm alisema hadi kufika
Jumatatu wachezaji wake wengi watakuwa wameunganika tayari kwa maandalizi
kuelekea mchezo wao ujao.
Jana
wachezaji wa Yanga waliendelea na mazoezi katika uwanja wa Boko Veterani, Dar
es Salaam, lakini Tambwe aliyekuwepo mazoezini hapo alikuwa mtazamaji huku
akiwa amefungwa kifaa tiba maalumu shingoni kutokana na matatizo ya shingo
yanayomkabili.
Akizungumza
na gazeti hili, Tambwe alisema huwa shingo wakati mwingine inamsumbua, ingawa
si kwa kiwango cha kuogopa. “Lakini naamini nitakaa vizuri tu baada ya kupata
matibabu,” alisema Tambwe.
Licha ya
Tambwe, wachezaji Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Haji Mwinyi na Oscar Joshua nao
jana walishindwa kufanya mazoezi kutokana na majeraha yanayowakabili. Walifanya
mazoezi mepesi kutokana na kuwa majeraha waliyopata wakiwa na timu ya Zanzibar
katika mashindano ya Chalenji yanayoendelea nchini Ethiopia.
Joshua
ameumia kifundo cha mguu. Akizungumzia hali zao daktari wa timu hiyo, Haruni
Ally alisema zinaendelea vizuri na anatarajia pengine Jumatatu watakuwa
wamepona na kujumuika kufanya mazoezi na wenzao isipokuwa Joshua.
“Wanaendelea
vizuri, Cannavaro na Mwinyi wapo kwenye tiba na hali zao zinaendelea kuimarika
na Tambwe shingo yake ina matatizo kidogo, lakini mpaka Jumatatu atakuwa kwenye
mazoezi pamoja na wenzake isipokuwa Joshua yeye anaweza kuuguza kifundo kwa
wiki mbili”, alisema Ally.
No comments:
Post a Comment