Aliyekuwa beki wa Coasta Union ya Tanga Tumba Swedi
akisaini mkataba kujiunga na Mbeya city.
|
Beki aliyechipukia
katika kikosi cha Azam Academy na kwenda kuwa nguzo muhimu katika kikosi cha
Coasta union ya Tanga Tumba Swedi amejiunga na Mbeya city kwenda kuimarisha
safu ya ulinzi ya kikosi hicho kilicho pata pigo la kufungia kwa nahodha wake
na beki wake kisiki Juma Nyoso.
Kwa taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa Mbeya city zinasema:
Aliyekuwa mlinzi wa kutumainiwa wa timu ya Coastal Union ya Tanga, Tumba Swedi Luo amejiunga na kikosi cha Mbeya City Fc.
Mapema jana kwenye ofisi la City zilizopo jengo la Mkapa Hall jijini hapa Swedi ametia sini kandarasi ya mwaka mmoja na nusu tayari kabisa kuitumikia timu yake mpya kwenye ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara na pia mashindano mengine.
Akizungumza mara baaada ya kutia saini kandarasi hiyo Swedi alisema kuwa amefurahi kujunga na timu ambayo imekuwa na hamasa kubwa kwenye mpira wa Tanzania bara tangu aliponda ligi kuu huku akiahidi kufanya kazi kwa uwezo wake wote aliojaaliwa na Mungu kwa lengo la kuisaidia City kupata mafaniio zaidi kwenye ligi kuu.
“Nimefurahi kujiunga na City, hii ni timu ambayo imekuwa na hamasa kubwa, tangu ilipopanda daraja imeleta changamoto nzuri na zaidi imekuwa timu ya ushindani na kutafuta mafanikio, hakika namshukuru mwenyezi mungu, hapa ni sehemu ambayo naweza kupata mafanikio zaidi, imani yangu kubwa ushirikino wa pamoja na niliowakuta hapa tutakuwa na mafanikio zaidi ya yale niliyokuta” alisema.
Tumba Swedi Luo kabla ya kujiunga na City alikuwa mchezaji wa Coastal Union kwa misimu miwili mfululizo akicheza jumla michezo michezo 36 na kuisaidia timu yake hiyo ya zamani kushika nafasi tano kwenye msimamo wa ligi kuu ya vodacom msimu uliopita.

No comments:
Post a Comment