MB DOG |
MKURUGENZI wa Kampuni ya Qs Entertainment, Joseph
Mhonda, amemtabiria makubwa msanii wa muziki wa kizazi kipya aliyepata kutamba
miaka kadhaa iliyopita, Mbwana Mohammed maarufu kama Mb Doggy, Mb Doggy
aliyewahi kutamba na nyimbo mbalimbali, ukiwamo Latifa, Si Uliniambia na
nyinginezo, alishuka kiwango kidogo, jambo linalomfanya sasa apiganie mafanikio
ili arudi tena kileleni.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mhonda
alisema kuwa Mb Dogg ni miongoni mwa wasanii wa kizazi kipya wanaoweza kukaa
chini na kuandika mashairi mazuri, hivyo kurudi kileleni ni jambo rahisi kwake.Alisema
anaamini wakati wowote ukifika ataanza kuwika tena katika vituo vya redio na
televisheni kwa kuachia nyimbo kali zenye kugusa kila mtu.
“Kwa msanii kama Mb Doggy anayeweza kuandika
mashairi wakati wowote na kugusa hisia za wengi kurejea kileleni ni kitu rahisi
mno kwake, hivyo naamini kwa sasa anajua kitu anapaswa kufanya.
“Naamini kila kitu kinafanyika vizuri kwa ajili ya
kumuona Mb Doggy aliyezoeleka kwa wadau wa muziki wa kizazi kipya, ingawa soko
la Bongo Fleva linazidisha ushindani kila wakati,” alisema.
Qs ndiyo kampuni inayofanya kazi na Mb Dogg na
wasanii mbalimbali wa muziki huo, akiwamo Ney wa Mitego anayetamba na wimbo wa
Muziki Gani, akimshirikisha msanii Nassib Abdulmalick, Diamond.
No comments:
Post a Comment