HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Sunday, 9 February 2014

CLICK HAPA KUPATA TAARIFA ZA LIGI ZA MAJUU



LIGI KUU ENGLAND: MAN UNITED YABANWA NA TIMU YA MKIANI FULHAM!

>>JUMATANO NI EMIRATES: ARSENAL v MAN UNITED!
MATOKEO:
Jumapili Februari 9
Tottenham 1 Everton 0
Man United 2 Fulham 2

+++++++++++++++++++++++++++++
MAN UNITED 2 FULHAM 2
MABINGWA wa England, Manchester United, licha ya kutawala Mechi yote, kukosa Nafasi nyingi mno na hata kuweza kutoka nyuma kwa Bao 1-0 na kumudu kuongoza kwa Bao 2-1 walikatwa maini katika Dakika ya 94 wakati Darren Bent aliposawazisha kwa Bao laini.
Ikiwa kinyume na Gemu ilivyokwenda, Fulham, ambao wako mkiani kwenye Ligi Kuu England, walipata Bao la kuongoza laini wakati Difensi ya Man United ilipomegeka na kumruhusu Sidwell kukatiza kati na kufunga.
Bao hilo lilidumu hadi Mapumziko.
Kipindi cha Pili, Man United walifanya mabadiliko kadhaa kwa kuwaingiza kina Valencia, Januzaj na Chicharito na hii ilileta uhai na waliweza kufunga Bao 2 katika Sekunde 90.
Lakini kosa kosa zao za kufunga Bao la 3 kuliwagharimu kwani bila kutarajiwa Bent aliisawzishia Fulham kwenye Dakika za Majeruhi na kupata Sare ya Bao 2-2.
+++++++++++++++++++++++++++++
Man Utd 2
-Robin van Persie Dakika ya 78
-Carrick 80
Fulham 2
-Sidwell Dakika ya 19
-Bent 90

+++++++++++++++++++++++++++++

Mechi inayofuata kwa Man United ni hapo Jumatano huko Emirates watakapoivaa Arsenal ambayo Jana ilikung’utwa Bao 5-1 na Liverpool huko Anfield.
VIKOSI:
MAN UNITED: De Gea, Rafael, Smalling, Vidic, Evra; Mata, Carrick, Fletcher, Young; Rooney, van Persie.
Akiba: Lindegaard, Ferdinand, Giggs, Valencia, Kagawa, Januzaj, Hernandez
FULHAM: Stekelenburg; Riether, Burn, Heitinga, Riise; Tunnicliffe, Sidwell, Kvist, Richardson; Holtby, Tankovic
Akiba: Stockdale, Hangeland, Kacaniklic, Duff, Cole, Parker, Bent
REFA: Kevin Friend

+++++++++++++++++++++++++++++

TOTTENHAM 1 EVERTON 0
Bao la Emmanuel Adebayor, la Dakika ya 65, limewapa ushindi wa Bao 1-0 Tottenham na kuishusha Everton toka Nafasi ya 5 na kukamata wao.
VIKOSI:
Spurs: Lloris, Walker, Dawson, Vertonghen, Rose, Bentaleb, Dembele, Lennon, Paulinho, Eriksen, Adebayor
Akiba: Kaboul, Soldado, Capoue, Naughton, Townsend, Defoe, Friedel.
Everton: Howard, Coleman, Jagielka, Distin, Baines, McCarthy, Barry, Naismith, Osman, Pienaar, Mirallas
Akiba: Robles, Hibbert, Stones, Traore, Deulofeu, Barkley, McGeady.
REFA: Mark Clattenburg
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
PTS
GD
1
Chelsea FC
25
17
5
3
47
20
27
56
2
Arsenal FC
25
17
4
4
48
26
22
55
3
Man City
25
17
3
5
68
27
41
54
4
Liverpool
25
15
5
5
63
30
33
50
5
Tottenham
25
14
5
6
32
32
0
47
6
Everton FC
25
12
9
4
37
26
11
45
7
Man United
25
12
5
8
41
31
10
41
8
Newcastle
25
11
4
10
32
34
-2
37
9
Southampton
25
9
9
7
36
29
7
36
10
Swansea
25
7
6
12
32
35
-3
27
11
Hull City
25
7
6
12
25
30
-5
27
12
Aston Villa
25
7
6
12
27
36
-9
27
13
Stoke City
25
6
8
11
26
40
-14
26
14
Crystal Palace
25
8
2
15
18
34
-16
26
15
West Ham
25
6
7
12
26
33
-7
25
16
Norwich City
25
6
7
12
19
37
-18
25
17
Sunderland
25
6
6
13
25
38
-13
24
18
West Brom
25
4
11
10
29
37
-8
23
19
Cardiff City
25
5
6
14
19
44
-25
21
20
Fulham FC
25
6
2
17
24
55
-31
20

RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumanne Februari 11
2245 Cardiff v Aston Villa
2245 Hull v Southampton
2245 West Ham v Norwich
2300 West Brom v Chelsea

Jumatano Februari 12
2245 Arsenal v Man United
2245 Everton v Crystal Palace
2245 Man City v Sunderland
2245 Newcastle v Tottenham
2245 Stoke v Swansea
2300 Fulham v Liverpool 
   

SERIE A: TEVEZ AIPA JUVE BAO 2, VERONA WACHOMOA!

TEVEZ

LICHA ya Juventus kutangulia kwa Bao 2 za mapema kupitia Carlos Tevez, Hellas Verona walirudisha Bao zote nakupata Sare ya Bao 2-2 walipocheza na Mabingwa hao wa Italy ambao pia ni Vinara wa Serie A huko Italy.
Luca Toni

Baada Tevez kupiga Bao 2, Luca Toni aliifungia Hellas Verona Bao la kwanza na Muargetina Juanito Gomez kusawazisha katika Dakika ya 94.
Baada ya hii Leo Timu ya Pili AS Roma nao kubanwa na kutoka Sare 0-0 Lazio, Juve wamebaki kileleni wakiwa Pointi 9 mbele ya AS Roma na wako Pointi 13 mbele ya Timu ya Tatu Napoli ambao waliifunga AC Milan 3-1 hapo Jana Jumamosi.
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Februari 8
Udinese 3 Chievo Verona 0
Fiorentina 2 Atalanta 0
Napoli 3 AC Milan 1
Jumapili Februari 2
Torino 1 Bologna 2
Lazio 0 AS Roma 0
Parma 0 Catana 0
Sampdoria 1 Cagliari 0
Livorno 0 Genoa 1
Hellas Verona 2 Juventus 2
2245 Inter Milan v Calcioa
MSIMAMO-Timu za Juu:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Juventus FC
23
19
3
1
56
18
38
60
2
AS Roma
22
15
6
1
45
11
34
51
3
SSC Napoli
23
14
5
4
47
27
20
47
4
Fiorentina
23
13
5
5
42
24
18
44
5
Hellas Verona
23
11
3
9
39
37
2
36
6
Inter Milan
22
8
9
5
39
27
12
33


No comments:

Post a Comment