HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Friday, 7 February 2014

CLICK HAPA UPATE TATHMINI YA MECHI ZA WIKIENDI LIGI KUU ENGLAND



>>BIGI MECHI JUMAMOSI: LIVERPOOL v ARSENAL
>>JUMAPILI: SPURS v EVERTON, MAN UNITED v FULHAM!
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Februari 8
1545 Liverpool v Arsenal
1800 Aston Villa v West Ham
1800 Chelsea v Newcastle
1800C rystal Palace v West Brom
1800 Norwich v Man City
1800 Southampton v Stoke
1800 Sunderland v Hull
2030 Swansea v Cardiff
Jumapili Februari 9
1630 Tottenham v Everton
1900 Man United v Fulham
+++++++++++++++++++++++++++++
LIGI KUU ENGLAND Jumamosi inaingia Mechi zake za 25 kwa kuanza na mtanange mkali kabisa huko Anfield wakati Wenyeji Liverpool watakapowakaribisha Vinara wa Ligi Arsenal.

IFUATAYO NI TATHMINI MECHI KWA MECHI:



LIVERPOOL V ARSENAL 



Hali za Wachezaji
Kwa mujibu wa Meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers, Liverpool itawakosa Majeruhi Daniel Agger, Mamadou Sakho, Jose Enrique na Glen Johnson huku Lucas Leiva akiwa na hatihati.
Arsenal itamkosa Mathieu Flamini ambae anatumikia Kifungo cha Mechi 3 na hii ni ya pili kwake na pia watamtathmini Jack Wilshere ambae alikuwa Majeruhi.

Tathmini ya Mechi
Ingawa Mwezi iliopita Brendan Rodgers alidai Liverpool itapigana hadi mwisho kugombea Ubingwa, hapo Juzi Meneja huyo wa Liverpool amekiri Ubingwa kwao ni nje na lengo kuu kwao ni kumaliza 4 Bora.
Wakiwa Nafasi ya 4, wakiandamwa na Everton, Tottenham na Man United, Liverpool hawana budi kupata matokeo mazuri kwenye Mechi hii na Arsenal ikiwa wana nia hasa ya kumaliza 4 Bora Msimu huu.
Lakini Liverpool wana kibarua kigumu maana Timu pekee ambayo iliweza kuwazuia Mastraika wao hatari, Luis Suarez na Daniel Sturridge, kutofunga Bao katika Mechi zao 12 za Ligi zilizopita ni Arsenal baada ya kuwachapa 2-0 huko Emirates hapo Novemba 2 kwenye Mechi ya Ligi.
Kwa Arsenal, Mechi hii ni moja kati ya Mechi zao ngumu kwa Mwezi huu Februari wanapokabiliwa na mtihani baada ya mtihani kwani baada ya hii wataivaa Man United kwenye Ligi huko Emirates, kisha Liverpool tena kwenye FA CUP na kufuatia Bayern Munich kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI na kumalizia Mwezi kwa Mechi ya Ligi na Sunderland.
Uso kwa Uso
-Liverpool wameshinda Mechi 1 tu kati ya 13 za Ligi walizocheza mwisho na Arsenal lakini 7 kati ya hizo ni Sare. (W1, D7, L5).
-Arsenal wanasaka ushindi wa 3 mfululizo Uwanjani Anfield.
-Mara ya mwisho kushinda mara 3 mfululizo ni kati ya Tarehe 10 Februar1 1973 na 9 Novemba 1974.
-Mechi za Timu hizi mbili kwenye Ligi Kuu England ndizo zimetoa Hetitriki nyingi kupita zote na zimeshafungwa Hetitriki 5 kwenye Mechi zao.



VIKOSI VINATARAJIWA:
LIVERPOOL: Mignolet, Flanagan, Skrtel, Toure, Cissokho, Sterling, Henderson, Gerrard, Coutinho, Sturridge, Suarez
ARSENAL: Szczesny, Sagna, Gibbs, Mertesacker, Koscielny, Arteta, Chamberlain, Rosicky, Ozil, Cazorla, Giroud
REFA: Michael Oliver

SUNDERLAND V HULL CITY
-Stadium Of Light
Hii ni Mechi inayozikutanisha Sunderland ambayo sasa imeimarika upya chini ya Meneja Gus Poyet na wapo Pointi sawa na Hull City ambao wametwaa Pointi 1 tu katika Mechi zao 5 zilizopita.
Lakini hiyo Pointi 1 ni kwenye Mechi ya Sare ya 1-1 na Tottenham ambayo Hull ilikuwa na Mastraika wapya, Shane Long and Nikica Jelavic, walioonekana hatari.
VIKOSI VINATARAJIWA: 
SUNDERLAND: Mannone, Bardsley, O’Shea, Brown, Alonso, Johnson, Ki, Colback, Borini, Altidore
HULL CITY: Harper, Rosenior, McShane, Davies, Figueroa, Elmohamady, Meyler, Huddlestone, Brady, Jelavic, Long
REFA: Mike Jones
SWANSEA CITY V CARDIFF CITY
-Liberty Stadium
Hii ni Dabi ya South Wales na Cardiff wana nafasi ya kuweka Rekodi ya kuwafunga Wapinzani wao mara mbili kwenye Msimu mmoja wa Ligi na hii ni nafasi kubwa kwani Jumanne Swansea walimtimua Meneja wao Michael Laudrup.
Kwa Mechi hii, Swansea itafundishwa na Nahodha wao Garry Monk ambae itabidi aichunge Cardiff ambayo Wachezaji wao wapya, Kenwyne Jones na Wilfried Zaha, wameonyesha kuwa hatari kubwa.
VIKOSI VINATARAJIWA:
SWANSEA: Tremmel, Tiendalli, Chico, Williams, Davies, DE Guzman, Amat, Dyer, Shelvey, Routledge, Bony
CARDIFF: Marshall, Fabio, Caulker, Turner, John, Noone, Medel, Bellamy, Whittingham, Mutch, Jones
REFA: Andre Marriner

ASTON VILLA V WEST HAM UNITED
-Villa Park
Huenda West Ham wakamkosa Straika wao Andy Carroll ambae amefungiwa Mechi 3 na Rufaa yake kutupwa lakini baada ya West Ham kutishia kuiburuza FA Mahakamani Chama hicho cha Soka England kimekubali Leo kusikilia upya Kesi hiyo.
Wakati West Ham wakiomba Mungu Carroll awepo, Aston Villa wanae Straika wao hatari Christian Benteke ambae sasa amerudi tena kuziona nyavu.
VIKOSI VINATARAJIWA:
ASTON VILLA: Guzan, Bacuna, Vlaar, Baker, Clark, Bertrand, Weimann, Westwood, Delph, Holt, Benteke
WEST HAM: Adrian, Demel, Collins, Tomkins, McCartney, Noble, Taylor, Jarvis, Nolan, Downing, Cole
REFA: Mike Dean

CHELSEA V NEWCASTLE UNITED
Stamford Bridge
Ni wazi ni ngumu kwa Newcastle kurudia kipigo cha Bao 2-0 walichoibonda Chelsea katika Mechi ya kwanza kati yao Msimu huu kwenye Mechi hii inayochezwa kwenye ngome ya Chelsea, Stamford Bridge, ambako Chelsea, chini ya Mourinho, hawajafungwa hata Mechi moja ya Ligi.
Kwenye Mechi hii, Newcastle watamkosa Straika wao hatari, Loic Remy, ambae yuko Kifungoni wakati Chelsea wanaweza kumpa Namba kwa mara ya kwanza Mchezaji wao mpya Mohamed Salah wa Egypt aliehamia kutoka FC Basel ya Uswsisi.
VIKOSI VINATARAJIWA:
CHELSEA: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Matic, David Luiz, Ramires, Willian, Hazard, Eto’o
NEWCASTLE: Krul, Debuchy, Williamson, Taylor, Santon, Anita, Tiote, Sissoko, Ben Arfa, Sammy Ameobi, Shola Ameobi
REFA: Howard Webb
CRYSTAL PALACE V WEST BROMWICH ALBION
-Selhurst Park
Tangu wakutane Mwezi Novemba, Timu hizi sasa zina Mameneja wapya.
Tony Pulis amefanikiwa kuiweka Crystal Palace kama Timu imara na ngumu ambayo huzoa Pointi kwa Timu za karibu yao kwenye Msimamo wa Ligi.
West Brom bado wanajivutavuta chini ya Meneja mpya Pepe Mel.
VIKOSI VINATARAJIWA: 
CRYSTAL PALACE: Speroni, Ward, Gabbidon, Delaney, Parr, Puncheon, Dikgacoi, Jedinak, Bolasie, Chamakh, Jerome
WEST BROM: Foster, Jones, McAuley, Olsson, Ridgewall, Mulumbu, Yacob, Berahino, Gera, Brunt, Vydra
REFA: Chris Foy

NORWICH CITY V MANCHESTER CITY
-Carrow Road
Norwich hawatabiriki kwani leo hucheza vizuri na Mechi inayofuata ni balaa kwao.
Hii ni Mechi ngumu mno kwao hasa kwa vile Man City wana machungu ya kupigwa Bao 1-0 Nyumbani kwao Etihad na Chelsea katika Mechi yao iliyopita.
VIKOSI VINATARAJIWA: 
NORWICH: Ruddy, Martin, Bennett, Bassong, Martin Plsson, Snodgrass, Tettey, Johnson, Guiterrez, Elmander, Hooper
MAN CITY: Hart, Zabileta, Kompany, Nastasic, Kolarov, Navas, Demichelis, Toure, Silva, Dzeko, Megredo
REFA: Jonathan Moss

SOUTHAMPTON V STOKE
-St Mary's Stadium
Stoke wanatinga Mechi hii wakiwa hawajashinda Ugenini tangu Mwezi Agosti na hii Mechi ni ngumu kwao kwa vile Southampton hupenda kushambulia kwa kujaza Watu kwenye Kiungo.
VIKOSI VITATOKANA NA:
SOUTHAMPTON: Boruc, K Davis, Gazzaniga, Clyne, Chambers, Shaw, Fox, Hooiveld, Fonte, Yoshida, Wanyama, Schneiderlin, Cork, Lallana, Isgrove, Ward-Prowse, Do Prado, S Davis, Reed, Rodriguez, Lambert.
STOKE: Begovic, Sorensen, Shawcross, Wilson, Pieters, Cameron, Muniesa, Shotton, Whelan, Adam, Palacios, Ireland, Assaidi, Nzonzi, Arnautovic, Walters, Crouch, Guidetti, Odemwingie
REFA: Craig Pawson
++++++++++++++++++++++++++++++++++
Jumapili Februari 9
TOTTENHAM V EVERTON
-White Hart Lane
Everton wanaingia White Hart Lane wakiwakosa Washambuliaji wao wakuu, Gerard Deulofeu na Romelu Lukaku, ambao ni Majeruhi.
Tottenham hupenda kushambulia kwa kundi na kurudi kundini kwa Kiungo Paulinho, aliekuwa majeruhi kitambo, kutasaidia kuimarisha kiungo chao wakati wa mashambulizi.
VIKOSI VINATARAJIWA:
TOTTENHAM: Lloris, Walker, Dawson, Vertonghen, Rose, Lennon, Bentaleb, Paulinho, Eriksen
EVERTON: Howard, Stones, Jagielka, Distin, Baines, McCarthy, Barry, McGeady, Barkley, Osman, Mirallas
REFA: Mark Clattenburg

MANCHESTER UNITED V FULHAM
Old Trafford
Fulham watamtumia Straika hatari wa Ugiriki, Konstantinos Mitroglou, kwa mara ya kwanza na kuimarishwa na Mchezaji mpya miwingine, John Heitinga, kwenye Difensi.
Man United huenda wakamchezesha Nyota Chipukizi Adnan Januzaj ambae hakucheza Mechi iliyopita.
VIKOSI VINATARAJIWA:
MAN UNITED: De Gea, Rafael, Smalling, Jones, Evans, Carrick, Cleverley, Januzaj, Rooney, Van Persie, Mata
FULHAM: Stockdale, Passley, Hangeland, Burn, Amorebieta, Kasami, Parker, Tankovic, Kacanikilic, Dempsey
REFA: Kevin Friend
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Arsenal FC
24
17
4
3
47
21
26
55
2
Manchester City
24
17
2
5
68
27
41
53
3
Chelsea FC
24
16
5
3
44
20
24
53
4
Liverpool
24
14
5
5
58
29
29
47
5
Everton FC
24
12
9
3
37
25
12
45
6
Tottenham Hotspur
24
13
5
6
31
32
-1
44
7
Manchester United
24
12
4
8
39
29
10
40
8
Newcastle United
24
11
4
9
32
31
1
37
9
Southampton FC
24
9
8
7
34
27
7
35
10
Aston Villa
24
7
6
11
27
34
-7
27
11
Stoke City FC
24
6
7
11
24
38
-14
25
12
Swansea City AFC
24
6
6
12
29
35
-6
24
13
Hull City
24
6
6
12
23
30
-7
24
14
Sunderland
24
6
6
12
25
36
-11
24
15
Norwich City
24
6
6
12
19
37
-18
24
16
West Bromwich
24
4
11
9
28
34
-6
23
17
Crystal Palace FC
24
7
2
15
15
33
-18
23
18
West Ham United
24
5
7
12
24
33
-9
22
19
Cardiff City
24
5
6
13
19
41
-22
21
20
Fulham FC
24
6
1
17
22
53
-31
19
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumanne Februari 11
2245 Cardiff v Aston Villa
2245 Hull v Southampton
2245 West Ham v Norwich
2300 West Brom v Chelsea
Jumatano Februari 12
2245 Arsenal v Man Unitwd
2245 Everton v Crystal Palace
2245 Man City v Sunderland
2245 Newcastle v Tottenham
2245 Stoke v Swansea
2300 Fulham v Liverpool

No comments:

Post a Comment