Meneja wa Uwanja wa Mkwakwani,Mbwana Msumari(kulia) nakatibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga (CCM)Gustav Muba wakizungumza na Waandishi wa habari katika moja ya vyumba vya kubadilishia nguo ambavyo pia vimefanyiwa maerekebisho |
Kutoka kushoto ni Meneja wa Uwanja wa
Mkwakwani,Mbwana Msumari akitoa ufafanuzi kwa katibu wa Chama cha Mapinduzi
Mkoa wa Tanga (CCM)Gustav Muba kuhusu maandalizi ya uwanja huo
|
SEHEMU YA KUCHEZEA BAADA YA KUPANDA NYASI MPYA |
HAYA NI BAADHI YA MAGETI YA
KIELECTRONIKI AMBAYO YALIFUNGWA KWENYE UWANJA WA CCM MKWAKWANI AMBAYO YATATUMIKA
KWENYE MECHI ZA LIGI KUU TANZANIA BARA.
|
Shirikisho
la Soka nchini TFF kwa kushirikiana na uongozi wa uwanja wa Mkwakwani
limejipanga kubaliana na changamoto zitakazojitokeza katika mchezo wa leo
kuhusiana na tiketi za Kielektroniki.
Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uwanjani hapo,Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF,Khalid Abdallah na katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Tanga,Gustav Muba walisema wamejipanga kukabiliana na changamoto hizo.
Khalid ambaye pia ni msimamizi wa ligi kuu Vodacom,kituo cha Tanga alisema baada ya kukamilika kwa matengenezo ya uwanja wa Mkwakwani kuna changamoto ambazo zitajitokeza kutokana na ukweli kwamba milango iliyoandaliwa ni miwili tu.
“Tatizo ni kwamba wawekaji wa mashine za kielektroniki wameweka mageti mawili tu ambayo kwa uzoefu ukataji wa tiketi hautatosheleza idadi ya mashabiki watakaoingia”alisema Khalid.

Mjumbe huyo hata hivyo aliwataka wapenzi kujitokeza kwa wingi bila kuhofia tatizo hilo kwa sababu,TFF na uongozi wa uwanja wamejipanga kuhakikisha kila atakayefika anaingia uwanjani kushuhudia mechi zitakazo pigwa katika Uwanja Huo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga alisema uwanja wa mkwakwani umekamilika marekebisho kwa asilimia kubwa na unaweza kuhimili kuchezewa ligi kuu bila matatizo.
No comments:
Post a Comment