Kikosi
cha Coastal Union kilichomenyana na JKT
Oljoro uwanja wa Mkwakwani
|
Meneja
wa Coastal Union akitaniana na Kocha wa JKT Oljoro Hemed Morocco kabla ya
mchezo
|
Atupele
Green akimtoka mchezaji wa JKT Oljoro uwanja wa Mkwakwani
|
Kenneth Masumbuko, akitafuta mbinu za kumtoka Nurdin Mohammed wa JKT Oljoro katika uwanja wa Mkwakwani |
Yayo
Kato Lutimba
|
TIMU ya
Coastal Union ya Tanga hapo jana ilishindwa kuutimia vema uwanja wake wa
nyumbani baada ya kulazimishwa sare na Oljoro JKT ya Arusha kwenye mechi ya
Ligi kuu Tanzania bara mzunguko wa pili.
Mchezo
huo uliochezwa kwenye dimba la soka Mkwakwani ulikuwa mkali na wenye upinzani
mkubwa ambapo mpaka timu zote zinakwenda mapumziko Coastal Union walikuwa
wakiongoza bao 1-0.
Bao
ambalo lilifungwa na Yayo Lutimba aliyeunganisha pasi nzuri iliyopigwa na
Hamadi Hamisi bao ambalo lilidumu mpaka timu zote zinakwenda mapumziko.
Kipindi
cha pili kilianza kwa kasi ambapo Coastal Union na Oljoro JKT waliingia kwenye
ngwe hiyo kwa kila timu kufanya mabadiliko kwenye kikosi chake.
Wakicheza
kwa kujituma na umakini mkubwa Coastal Union waliweza kutawala mchezo huo mpaka
dakika ya 75 ya kipindi cha pili ambapo nao wapinzani wao walipocharuka.
Baada ya
kucharuka Oljoro JKT waliweza kucheza pasi fupi fupi na ndefu wakitumia udhaifu
wa wapinzani wao na ndipo walipofanikiwa kuandika bao la kusawadhisha kwenye
dakika ya 87 kupitia Hamis Salehe.
Hata
hivyo mechi hiyo ilikuwa haina mashabiki wengi kwa kile kilichoelezwa kuwa
mfumo wa kielectroniki ulichangia kuwepo kwa hali hiyo.
KIKOSI CHA COASTAL UNION gk Said Lubawa,Hamadi
Hamisi,Othumani Tamimu,Juma Nyoso,Jerry Santo,Mbwana Hamisi,Atupele
Green,Razack Khalifani,Yayo Lutimba,Daniel Lyanga na Keneth Masumbuko.
Kwa
upande wa JKT Oljoro gk Mohamed Ally,Paul Malipesa,Ally Omari,Nurdin
Mohamed,Sabri Makame,Babu Ally,Jacob Massawe,Azizi Shaweji,Amiri Omari,Shija
Mkina na Majaliwa Shabani.
Michezo
mengine iliyochezwa kwenye ligi hiyo ni Ashanti United walicheza na Yanga
ambapo mpaka dakika 90 Yanga 2-1 Ashanti United.
Mabao ya
Yanga yakifungwa na Didier Kavumbangu na David Luhende dakika ya 51 na 82 na la
Ashanti United limefungwa Bright Obinna dakika ya 61
Kwenye
dimba la Chamazi,Azam Fc waliibika na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar
bao likifungwa na Kipre Tchetche.
Hali
kadhalika Mbeya City nao waliibuka na ushindi wa Bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar
kwenye dimba la soka Katiba Bukoba bao hilo likifungwa na Swita Julius
No comments:
Post a Comment