HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Tuesday, 28 January 2014

MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO AWAPA KAZI MGAMBO


MKUU wa wilaya ya Lushoto,Alhaj Majid Mwanga


Na Oscar Assenga,Lushoto.
MKUU wa wilaya ya Lushoto,Alhaj Majid Mwanga amewataka vijana walihitimu mafunzo ya mgambo kata ya Lukozi Tarafa ya Mlalo wilayani humo kufuatilia na komesha vitendo vinavyofanywa na vijana vya kuwapa mimba wanafunzi kike  pamoja na kuwakamata wazazi wanaowaozesha watoto wao wakiwa bado mashuleni.

Mwanga alitoa agizo hilo jana wakati akifunga mafunzo ya mgambo ya  miezi sita kata ya Lukozi Tarafa ya Mlalo kwa wahitimu wapatao 99 ambapo kati yao wa kike watano na wakiune tisini na nne.

Alisema wahitimu hao wana jukumu kubwa la kuhakikisha pia
wanalidhibiti suala la utoro kwa wanafunzi pamoja na kutoa elimu juu ya athari za ukimwi na rushwa katika maeneo mbalimbali wilayani humo.

Mkuu huyo wa wilaya alisema suala lengine ambalo wanapaswa kulitia mkazo mkubwa ni kuwaeleza vijana wengine mafanikio yaliyoyapata wakati wa mafunzo  hayo ikiwemo kulinda vyanzo vya maji na misitu.

Aidha aliwataka vijana hao kushiriki katika shughuli mbalimbali za
maendeleo kama ujenzi wa maabara pamoja na kuwa mstari wa mbele kuzuia vitendo viovu kwenye jamii zao ikiwemo wizi,uporaji.

Hata hivyo DC Mwanga aliwataka wahitimu hao kuwa mabalozi wazuri  kwenye familia zao kupitia kauli mbiu ya Jeshi la Polisi Tanzania ya kuwa “Katika familia yangu hakuna uhalifu na  Utii wa sheria bila shuruti n wa kila mwananchi na kila kiongozi.

No comments:

Post a Comment